Waziri wa maji Jumaa Aweso akiwa na wadau wa sekta ya maji katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo ya maji Auwsa. 

Mwenyekiti wa bodi ya maji Auwsa Dr Richard Masika, Akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo wakati wa uzinduzi wa bodi ya maji jijini Arusha.




Jane Edward, Arusha


Waziri wa maji Jumaa Aweso amemwagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Injinia Anthony Sanga kutoa kiasi cha sh,bilioni 1 kwaajili kutatua changamoto za maji eneo la Namanga ili kuondoa adha wanazopata wananchi kununua maji



Aweso alitoa maagizo hayo wakati wa  uzinduzi wa bodi ya tisa ya wakurugenzi wa Mamlaka hiyo katika ofisi mpya za Kanda zilizoko Mkoani Arusha. 



Alisema ni lazima tathimini za miradi ya maji zifanyike kwa uhalisia ili kuondoa gharama kubwa za miradi na kuwezesha kuokoa fedha na kuibua miradi mingine



Alisisitiza bodi hiyo ya Auwsa kuboresha mazingira ya wafanyakazi kwani wafanyakazi wa Auwsa wanafanya kazi kubwa katika kuhakikisha mapato yanakua ikiwemo utoaji huduma bora kwa wananchi



Ameongeza wananchi wa Namanga wanapata tabu ya maji hivyo kutolewa kwa fedha hizo kutawezesha wananchi kupata maji na kuwezesha wananchi kupata maji katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha na Mkoa mzima



Alisema serikali ilipoamua kutoa fedha kwaajili ya mradi mkubwa wa maji sh, bilioni 520 ni vyema katika kuhakikisha wananchi wanapata maji na kusisitiza maslahi ya wafanyakazi yaboreshwe ili kuwezesha mafanikio kuwepo



"Naomba bodi isimamie nidhamu ya watumiaji ,nawaomba wananchi wapate huduma bora , wananchi wanatumia muda wao kupiga simu na kuelezea tatizo lao watumishi hao waende kutatua kero zao"



Alimpongeza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwsa)Injia Justine Rujomba kwa kufanya kazi kubwa na kusimamia vema miradi ya maendeleo sanjari na kutatua kero kwa wananchi 



Alisisitiza huduma za mita za prepaid ziwekwe kwa wateja wakubwa na taasisi mbalimbali na kusisitiza gharama za uunganishaji wa maji ziwe kwa bei nafuu ili makusanyo yaweze kuongezeka




Aliagiza menejimenti na wafanyakazi wa mamlaka hiyo,kutoa ushirikiano kwa bodi hiyo ili kutimiza majukumu yao



Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Auwsa,Injinia Justine Rujomba alisema mamlaka hiyo ina vyanzo vya maji vya aina tatu ambavyo ni chemchem,mito na visima virefu na makusanyo yakipaa kutoka  bilioni 1 .8mwaka 2018 na kufika sh, bilioni 1.8



Pia Injia Rujomba alisema mwaka 2021 /26 wanampango wa kutafiti ujenzi wa matenki ya maji taka  na kutenga kiasi cha sh, bilioni 1.25 kwaajili ya uboreshaji wa huduma za maji katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Usariver



Naye  Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo alisema wananchi wa jimbo hilo wanapata maji na alimshukuru Mkurugenzi wa  Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwsa) Injia, Justine Rujomba kwa ushirikiano wake katika miradi ya maji



Alisema maeneo ya pembezoni shida ya maji ni kubwa haswa kata ya Olasiti,Teratt,Nadosoito na maeneo mengine bado yanachangamoto za maji na pia gharama za uunganishaji wa maji ni kubwa



Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Sophia Mjema alisisitiza maeneo ya pembezoni yaangaliwe ili wananchi waweze kupata maji safi na salama na kuipongeza mamlaka hiyo kuendelea kutoa huduma za maji kwa wananchi na kutatua changamoto haswa maeneo ya pembezoni



Naye  Mwenyekiti wa Bodi,Dk,Richard Masika alimhakikishia Waziri Aweso kuwa hawatamwangusha na watahakikisha wananchi wanapata maji na alikabidhi taarifa ya utendaji wa bodi hiyo iliyomaliza muda wake na kuteuliwa upya na kushukuru kwa uteuzi huo wa mara ya pili kwakuaminiwa katika utendaji wao wa Kazi



Alisema bodi itatekeleza majukumu yake vema katika kusimamia mpango wa biashara wa mwaka 2020/25,ilani ya uchaguzi  na ipo katika hatua za mwisho za utekelezaji wa huduma za maji safi na salama na kufika lita milioni 200,000 



Alitoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa walinzi wa vyanzo vya maji na kutoa taarifa za uharibufu wa miundombinu


Mwisho

Share To:

Post A Comment: