Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu.

Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watumishi sita wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa na aliyekuwa DED wa Halmashauri hiyo ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo, Asajile Mwambambale kwa tuhuma ya wizi wa mabati 1,172 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 31.

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 24, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu, na kusema kwamba mabati hayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye stoo ya halmashauri hiyo na katika wizi huo hakuna kufuli wala mlango uliovunjwa.

Share To:

Post A Comment: