Saturday, 14 August 2021

DED MKURANGA MWANTUM MGONJA AKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI

 

Mkurugenzi Mtendaji  Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Ndg.Mwantum Mgonja ameungana na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mkuranga kukagua Miradi ya Maendeleo iliyopo Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.


Ndugu Mwantum Mgonja ambaye pia ndiye Mtendaji Mkuu wa kutekeleza Miradi hiyo na fedha za utekezaji zikiwa zimetoka ndani ya Halmashauri ya  Mkuranga pamoja na Serikali Kuu,ameongozana na Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo kukagua Mradi wa Shule Sekondari Nasibugani Kata ya Msonga, Zahanati ya Nganje Kata ya Mgawa, Shule ya Sekondari Kisiju  Kata ya Dondo.

Vilevile  Mkurugenzihm huyo ametembelea Kituo cha Afya cha Kisiju Kata ya Kisiju.

Hata hivyo ameshuhudia ujenzi wa Daraja Kata ya Shungubweni sambamba na ujenzi wa Mradi wa Maji kata ya Mbezi. 

Baada ya Ziara hiyo na kujionea hali halisi Ndg. Mwantum amesema kwenye miradi ambayo bado ipo kwenye ujenzi wahakikishe inakamilika kwa wakati uliopangwa na mwisho aliwataka wote wanaohusika na miradi hiyo kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano wa hali ya juu,ili kuendelea kumsaidia Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

 Imetolewa na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya MkurangaNo comments:

Post a Comment