MKUU wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Halima Bulembo amehitimisha ziara yake katika Tarafa ya Amani yenye Kata Sita na Vijiji 24 iliyokua na lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za Wananchi wa maeneo hayo.

DC Bulembo amesema ziara yake hiyo imekua na mafanikio makubwa kwani imemfanya kufika katika vijiji vyote ambapo pamoja na kusikiliza kero na changamoto za wananchi hao pia alizipatia ufumbuzi.

" Leo tumehitimisha ziara   katika Tarafa ya Amani ambapo tumemaliza kata ya kisiwani yenye vijiji vitano ambavyo ni Kijiji cha Magoda, Kwemdimu, Kisiwani, Shembekeza na Mashewa, tunawashukuru wananchi waliojitokeza na hakika changamoto zimepatiwa ufumbuzi," Amesema DC Bulembo.

Kupitia ziara hiyo, DC Bulembo ameweza kujionea vivutio ambavyo Wilaya ya Muheza inavyo ambapo amewakaribisha wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini kufika katika milima ya Amani na kufanya utalii wa ndani.

Wilaya ya Muheza ina Tarafa nne ambapo baada ya DC Bulembo kumaliza Tarafa ya Amani sasa ziara hiyo inaendelea katika Tarafa ya Bwembwera kazi ikiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi hao.






Share To:

Post A Comment: