Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba (katikati) akizungumza na wajumbe wake wakati wakikagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama jana. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko na kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo ya Mkalama Sophia Kizigo.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Lucy Shee akizungumza kwenye ukaguzi huo.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua Hospitali ya Wilaya ya Mkalama.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akizungumza kwenye ukaguzi huo.

Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ukiendelea.

Mjumbe wa Halmashauri  Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita akizungumza kwenye ukaguzi huo.

Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ujenzi wa mradi wa maji.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ujenzi wa mradi wa maji.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakipokea taarifa ya ukarabati wa vyumba vya  maabara Shule ya Sekondari ya Gumanga.

Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ukarabati wa vyumba vya maabara Shule ya Sekondari ya Gumanga.
Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Singida wakikagua ujenzi wa  vyoo.
 


Na Dotto Mwaibale, Mkalama.

KAMATI  ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida imefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama  na kukagua utekelezaji wa Ilani kwenye miradi ya maendeleo.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Alhaji Juma Kilimba  akiwa ameambatana na wajumbe wake aliipongeza Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa utekelezaji wa miradi.

Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba sita za wakuu wa idara, ujenzi wa uzio kuzunguka ofisi za Halmashauri urefu wa mita 750, ujenzi wa madarasa mawili na vyoo ,matundu 12 Shule ya Sekondari Gumanga, ukamilishaji wa vyumba viwili vya maabara Sekondari ya Mpambala, mradi wa maji Kijiji cha Nkungi.

Mradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni upanuzi wa wodi ya watoto kwa gharama ya Sh.180 milioni, wodi ya wanawake 160 milioni na wodi ya wanaume 160 milioni katika Hospitali ya Wilaya.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisikitishwa na ukarabati wa vyumba vya maabara katika Shule ya Sekondari Chemchemi ambavyo vimejengwa chini ya kiwango ukilinganisha na vile vilivyokarabatiwa kwa Sh.25 milioni  katika Shule ya Sekondari ya Gumanga licha ya kutolewa Sh.35 milioni kwa kila shule kwa ajili ya ukarabati huo.

Alisema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo hivyo kuna kila sababu ya kuzitumia vizuri kwa manufaa ya wananchi.

Katika ziara hiyo viongozi mbalimbali walikuwepo wakiwemo wakuu wa idara wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo ya Mkalama Sophia Kizigo.

Leo  kamati hiyo itafanya ziara ya namna hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida

Share To:

Post A Comment: