Na Mwandishi wetu


NAIBU Waziri Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb) ameshiriki mkutano wa ishirini na nane (28)wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Bonde la Mto Nile Ukanda wa Maziwa Makuu ukijumuisha nchi tisa kati ya kumi zinazozunguka bonde la mto Nile ulioanzia Ziwa Victoria na kuishia nchini Misri mkutano uliofanyika Addis ababa Ethiopia.


Lengo la mkutano huo ni kujenga mahusiano ya kidiplomasia pia kulinda maslahi ya nchi zinazotumia maji kutoka Ziwa Victoria na Mto Nile.


Tanzania inanufaika na miradi ya kufua umeme ambapo pia huzalisha ajira lakini pia nchi hujenga diplomasia ya kiuchumi na nchi nyingine.


Aidha sababu nyingine ya mawaziri kukutana ni kutoa fursa nchi hizo kufungua njia za kiuchumi sambamba na kuibua miradi ya umeme kupitia mito iliyopo katika nchi hizo.


Hata hivyo katika hotuba  yake Naibu Waziri wa Maji Mhandisi ,Maryprisca Mahundi ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mwasiti Rashid   kutoka Balozi ya Tanzania Afisa Mratibu Vyanzo vya Maji Utawala na Maendeleo aliyechaguliwa kuongoza  nchi hizo na kwamba ana imani ataiwakilisha vema Tanzania kutokana na uzoefu alionao katika sekta ya Maji.


Amesema kutokana na janga la corona ni vema nchi zikatumia wataalaam wa ndani ili kuifanya miradi hiyo kwa wakati na ufanisi mkubwa.


Nchi zilizohudhuria mkutano huo ni pamoja na Burundi,D.R. Congo,Ethiopia,Kenya na Rwanda.


Nyingine ni Sudan ya Kusini,Sudan,Tanzania na Uganda.


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: