George Mwakang'ata (38) Mkazi wa Mbagala Kuu, Andrew Paul (34) Mkazi wa Kurasini na Said Mugoha (45) Mkazi wa Mtoni Kijichi Temeke wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri kusikiliza mashtaka yanayowakabili.
Wakati wa Wilaya ya Temeke wakiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam.

WAKAZI watatu wa Mkoani wa Dar es Salaa wamefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 1.02.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Yusuph Aboud imewataja washtakiwa hao kuwa ni ni George Mwakang'ata (38) Mkazi wa Mbagala Kuu, Andrew Paul (34) Mkazi wa Kurasini na Said Mugoha (45) Mkazi wa Mtoni Kijichi Temeke.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ritha Tarimo imedaiwa Juni 21,2021 huko Mivinjeni ndani ya Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, walisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine kilo 1.2 huku wakijua ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida kusikilizwa mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 27 mwaka huu itakapotajwa tena.

Share To:

Post A Comment: