Tuesday, 27 July 2021

SHIRIKA LA NYUMBA LATAKIWA KUTOA KIPAMBELE KWA MIKOA YA PEMBEZONI KUJENGA NYUMBA ZA MAKAZI

 

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula ameelekeza Shirika la Nyumba la Taifa NHC) kuipa kimpaumble mikoa ya pembezoni kwa kujenga nyumba za makazi ili kuwawezesha wananchi pamoja na watumishi wenye uhitaji.

Amewaelekeza kuwasiliana na viongozi wa mikoa hiyo ambayo pia imepakana na nchi jirani ili waweze kujenga nyumba hizo za makazi katika mikoa hiyo.

Mabula ametoa maelekeo hayo leo Julai 27,2021 mkoani hapa wakati akizindua nyumba nafuu za makazi zilizopo kata ya Mapupa Wilayani Masasi. Aliitaja baadhi ya mikoa ya pembezoni kuwa ni Kigoma, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Mabula amesema kuna uhitaji mkubwa sana wa nyumba za makazi kwa mikoa mingi hasa ya pembezoni huku akimuelekeza Mwenyekiti wa Bodi kuhakikisha wanaelekeza nguvu zaidi katika kujenga nyumba kwenye mikoa ya pembezoni.

“Kweli nimeona kuna hitaji kubwa la nyumba za makazi na hasa kwa mkoa wa mtwara, na mimi nielekele shirikka la nyumba, mwenye kiti wa bodi upo hapa, , mikoa mingi iliyoko pembezoni ina shida sana ya nyumba za makazi, na nyinyi ni shirika pekee ambalo tunalitegemea na kutarajia kwamba litapunguza kero za nyumba,” amesema .

Ameongeza Serikali inatarajia kuona kwamba shirika hilo kujenga walau nyumba sio chini ya laki mbili kwa mwaka Hulu akifafanua  shirika hilo halijaweza kufikia idadi hiyo huku akisisitiza waongeza nguvu kwa kuwapa kipaumbele mikoa ya pembezoni ili kuwawezesha wakazi wa maeneo ya mikoa hiyo wakiwemo watumishi wa umma kupata nyumba za makazi.

“Watumishi wengi wana hofu ya kwenda kufanya kazi katika mikoa hiyo kwa sababu hawana makazi na hata wakipata makazi wankuwa mbali na eneo la kazi, kwa hiyo ni vizuri mkawekeza katika maeneo hayo na mkaanza na mikoa ambayo imeshaomba huduma hiyo ifanyike,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mabula amepongeza na kushukuru shirika hilo kwa kazi kubwa wanayoifanya na za viwango nchini.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo, Mkurungezi Mkuu wa Shirika hilo Dk Maulid Banyani amesema shirika hilo limejenga nyumba hamsini na nne zenye thamani ya shilingi bilioni mbili. Amesema nyumba nyumba hizo ni za kisasa kila moja ikiwa na vyumba vitatu.

Amesema nyumba hizo ambazo zimejengwa kwa kutumia matofali maalumu zinapangishwa kila moja kwa shilingi laki moja na nusu na kwamba zimekwisha kupangishwa zote.

Kwa upande mwingine Dk.Banyani ameomba serikali iliwezeshe shirika hilo ili waweze kuendelea kujenga nyumba nafuu za makazi kwa wananchi huku akisema shirka hilo linaendelea kufanya jitihada zaidi kujenga nyumba nafuu kwa mikao mbalimbali nchini.

Amesema kwa Mkoa wa Mtwara, shirika hilo limeweza kujenga kutekeleza miradi ya nyumba yenye thamani ya shiling bilioni kumi na tisa.

No comments:

Post a Comment