Tuesday, 20 July 2021

NAIBU WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA MITAMBO YA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU NA RUVU CHINI

Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu Mhandisi Edward Mkilanya akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi(wa pili kulia)  kuhusu  mchakato wa uzalishaji wa maji unavyofanyika kwenye Mtambo wa maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara yake ya kutembelea mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Juu iliyokuwa na lengo la kuona miradi inayotekelezwa na DAWASA.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi  akinywa maji ya yanayozalishwa kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu ili kutambua ubora wa maji hayo  kukagua  miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akisaini kitabu cha wageni alipofika kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA ili kujionea ufanisi wa Miradi hiyo na kuweza kufikia malengo ya Serikali ya kumtua mama ndoo kichwani.

 Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi leo amefanya ziara kwenye mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ili kuona ufanisi wa miradi hiyo ya maji ya DAWASA.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara Mhandisi Mahundi amesema kuwa Serikali imeshaanza kusambaza Mita za maji za kulipia kadri ya matumizi   husika yaani Pre Paid Meter ili kuondoa Changamoto  mbalimbali ikiwa ni pamoja na bili bambikizi.

Mhandisi Mahundi amesema kuwa wamefika hatua ya kuanza matumizi ya mita hizo kufuatia malalamiko ya  Wananchi ambao wanadai kuwa wanabambikiziwa Bili kubwa kuliko matumizi yao jambo ambalo ni kinyume na inavyotakiwa.

 Mahundi amesema kuwa watahakikisha ifikapo 2025 upatikanaji wa maji safi katika maeneo ya mijini  unafikia asilimia 95 huku Vijijini ikifika asilimia 85.

Pia Mhandisi Mahundi ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) chini ya Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kwa kuendelea kutoa huduma ya maji pamoja na utandikaji wa mabomba sehemu zote ambazo maji hajafika maana kufanya hivyo wanapunguza tatizo la upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Naye Mkurugenzi wa Uzalishaji Na Usambazaji Maji Dawasa Shaban Mkwanywe ametolea   ufafanuzi maeneo ambayo yanahudumiwa na Mtambo  wa Ruvu Chini pamoja  Ruvu Chini na namna walivyojipanga kuwafikishia wananchi huduma ya maji kwenye Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Huu ni mwendelezo wa  wa serikali kuhakikisha  inaondoa Changamoto Ya Upatikanaji wa Maji Katika Maeneo mbalimbali Nchini. Hivyo DAWASA wamejipanga kuweza kumaliza changamoto ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe akimkaribisha pamoja na kumpa utangulizi Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi(wa kwanza kushoto) kuhusu Mtambo wa Ruvu Juu unavyofanya kazi wakati wa Ziara ya Naibu waziri alipotembelea Mtambo huo pamoja na kujionea ufanyaji kazi wake.
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu Mhandisi Edward Mkilanya akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi(wa pili kulia)  kuhusu  mchakato wa uzalishaji wa maji unavyofanyika kwenye Mtambo wa maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara yake ya kutembelea mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Juu iliyokuwa na lengo la kuona miradi inayotekelezwa na DAWASA.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi  akiendelea na ziara yake kwenye Mtambo wa Ruvu Juu
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza Ziara yake kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini na kujione unavyofanya kazi kwa ajili ya kumtua  ndoo mama mtoni wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi  akitembelea maeneo mbalimbali ya chanzo cha Maji Ruvu Chini kilichopo wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kukagua  miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA

Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini DAWASA Mhandisi Emaculata Paul akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyojipanga kutoa huduma ya usambazaji wa maji kwa kutumia eneo la mto huo kwa ajili ya upatikanaji wa maji mengi yatakayoweza kutumiwa na wananchi wa Dar es Salaam pamoja na Bagamoyo wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb).
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu DAWASA walivyojipanga kusambaza maji katika mikoa ya Dar es Salaam pamoja na Pwani wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi alipotembea mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini 
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza Ziara yake kwenye Mtambo wa Ruvu Chini na kufurahishwa na kazi inayofanywa na DAWASA katika usambazaji wa maji kwa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Pwani.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza jambo na Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini DAWASA Mhandisi Emaculata Paul alipotembelea
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi(kushoto) akizungumza jambo na Ziara ikiendelea

No comments:

Post a Comment