Monday, 5 July 2021

Naibu Waziri MaryPrisca Mahundi atembelea jengo la Machifu

 


Na Mwandishi wetu,Mbeya

NAIBU  Waziri wa Maji na Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea ujenzi wa jengo la machifu lililopo eneo la Nane Nane Jijini Mbeya.

Awali Chifu Roketi Mwanshinga alieleza maendeleo ya ujenzi akibainisha kusuasua kutokana na ukosefu wa fedha.

Katika kuwaunga mkono machifu Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi amejitolea malumalu za jengo lote ili jengo liwe na muonekana mzuri na wa kuvutia.
No comments:

Post a Comment