Mkuu
wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude, kushoto, akimkabidhi Mwenge
wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Tayari kwa
kukimbizwa wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiushika Mwenge wa Uhuru tayari kwa kukimbizwa wilayani humo leo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, akiushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, akiushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Christina Mzava, akiushika Mwenge wa Uhuru.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zikianza wilayani Shinyanga kwa kukagua miradi na kuweka jiwe la msingi.
Kiongozi
wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akikagua
ujenzi wa Maabara ya Sayansi katika shule ya Sekondari Mwalukwa.
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akiweka Jiwe la Msingi katika Zahanati ya Bushushu.
Muonekano wa Jengo la Zahanati ya Bushushu.
Kiongozi
wa Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi, akiweka
Jiwe la Msingi katika Nyumba za Watumishi mkoani Shinyanga zilizopo
Negezi Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa nyumba za watumishi.
Kiongozi
wa Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akiweka
jiwe la msingi katika Jengo la Uthibiti ubora wa Shule Kanda ya
Magharibi.
Muonekano wa Jengo la Uthibiti ubora wa Shule Kanda ya Magharibi.
Mbunge
wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vija na Ajira, akifungua maji
katika mradi wa maji Masekelo wa mtandao wa Ziwa Victoria ambao
ulitembelewa na Mwenge wa Uhuru kuona maendeleo yake ya utoaji huduma
kwa wananchi.
Koplo
Rehema Ali Haji ambaye ni Miongoni mwa viongozi wa Mbio Maalum wa
Mwenge wa Uhuru, akimtwisha ndoo ya Maji Mbunge wa Jimbo la Shinyanga
Mjini Patrobas Katambi, kwenye mradi huo wa maji wa Masekelo
unotekelezwa na Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga
(SHUWASA.)
Ukaguzi wa mfumo wa TEHAMA katika Shule ya Sekondari Uhuru ukiendelea na viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Awali
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kushoto Jasinta Mboneko, akiwa na Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi katikati
wakiendelea na ukaguzi wa miradi.
Kiongozi
wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi, ameweka
mawe ya msingi na kuona miradi mbalimbali ya maendeleo Wilaya ya
Shinyanga (Manispaa ya Shinyanga na wilaya ya Shinyanga), ambapo
ameridhishwa na miradi hiyo na hakuna ambao ameukataa.
Zoezi
la Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru kitaifa wilayani Shinyanga
limefanyika leo Jumapili Julai 11,2021 mara baada ya Mkuu wa wilaya ya
Kishapu Joseph Modest Mkude, kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga
Jasinta Mboneko katika viwanja wa michezo Shule ya Sekondari Mwalukwa
wilayani humo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi yote sita Luteni
Mwambashi amesema ameridhishwa na miradi hiyo ambayo imeendana na
thamani ya fedha (Value for Money), huku kukiwa na salio la fedha kwenye
baadhi ya miradi, na kuagiza ile ambayo haijakamilika kujengwa
ikamilishwe haraka ili ianze kutoa huduma.
“Nimekagua
miradi yote iko vizuri, na nimeweka jiwe la msingi, na ile ambayo
nimetoa maelekezo yafanyiwe kazi, pamoja na kuikamilisha ile ambayo bado
ipo kwenye hatua ya ujenzi ili itoe huduma haraka kwa wananchi,”amesema Luteni Mwambashi.
Pia
amewapongeza wananchi wa Bushushu kwa kujitoa kuchangia ujenzi wa
Zahanati, ambayo itawasaidia kuondokana na adha ya kufuata huduma za
matibabu umbari mrefu.
Akitoa
ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2021, amewataka Watanzania, kudumisha
amani, kuendeleza mapambano ya Rushwa, madawa ya kulevya, virusi vya
Ukimwi, Malaria, kuzingatia lishe bora kwa watoto, pamoja na Halmashauri
kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kieletroniki.
Kwa
upande wao Wabunge wa Shinyanga, akiwamo Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed
Salum, Patrobas Katambi Jimbo la Shinyanga mjini, pamoja na Christina
Mzava wa viti maalum, kwa nyakati tofauti waliahidi kuendelea kuwaletea
maendeleo wananchi, pamoja na kukamilisha maboma yaliyosalia kujengwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisoma taarifa ya mbio za
Mwenge wa Uhuru wilayani humo, amesema umekimbizwa Kilomita 136, pamoja
na kukagua miradi sita yenye gharama ya Sh. milioni 855.
Ameitaja
miradi hiyo kuwa ni, Ujenzi Maabara ya Sayansi katika shule ya
Sekondari Mwalukwa, Zahanati ya Bushusu, Nyumba nne za watumishi, Jengo
la Uthibiti ubora wa shule Kanda ya Magharibi, chumba cha Tehama katika
Shule ya Sekondari uhuru, pamoja na kuona maendeleo ya mradi wa maji
Ziwa Victoria Masekelo.
Katika
hatua nyingine Mboneko amewashukuru wananchi wa Shinyanga, kujitokeza
kwa wingi kwenye mbio hizo za Mwenge wa uhuru, huku akiwataka kuendelea
kushirikiana na Serikali kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2021 inasema “Tehama ni msingi wa Taifa endelevu, Itumike kwa usahihi na uwajibikaji"
Post A Comment: