Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati John Nchimbi ametoa muda wa siku Saba kwa mtendaji wa kijiji cha Dudiye kusoma mapato na matumizi kwa wananchi. 


Akizungumza katika mkutano wa mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sllo katika Kata ya Arri amesema baada ya tarehe 20.7.2021 hatosita kumfuta Kazi mtendaji wa kijiji hicho.

Amesema endapo mtumishi katika wilaya ya Babati atabainika kutumia vibaya madaraka yake hatosita kumchukulia hatua za kinidhamu.

Amesema pesa za wananchi zinatokana na nguvu mbalimbali hivyo wanaumia endapo hawasomewi Mapato na matumizi ya fedha zao.

Amemuahidi Mbunge kuwa yupo tayari kupokea maelekezo yatakayotolewa na ofisi yake wakati wote.

Mbunge wa Jimbo hilo amewataka viongozi wa serikali wawatumikie wananchi ili waendelee kushirikiana na serikali yao.

Wananchi wanadai kuwa zaidi ya mwaka mmoja hawajapewa taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji.
Share To:

Post A Comment: