Saturday, 10 July 2021

Masanja awataka wananchi watembelee Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja akipata maelezo Kutoka kwa Mkuu Ketengo Cha Mali kale na Idara ya Mawasiliano wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mwita William wakati Naibu Waziri alipotembelea banda la Wizara hiyo katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja akipata maelezo kutoka kwa Mrajisi wa Chuo cha Utalii Laurent kaheta wakati Naibu Waziri alipotembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja akipata maelezo kutoka kwa Afisa Utalii wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Naomi Mbilinyi wakati Naibu Waziri alipotembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.Picha mbalimbali katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja amesema wananchi watembelea banda la Maliasili katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba kujionea vitu mbalimbali vya Utalii na Maliasili.

Masanja ameyasema wakati wa Maonesho ya Sabasaba alipotembelea banda la Maliasili . amesema kuwa banda hilo limesheheni vitu vingi ikiwemo vile Historia ambapo wananchi wataona Mali kale ,wanyama na ndege ambao wapo Tanzania tu.

Wakati akitembelea sehemu mbalimbali amewataka wananchi kujifunza masuala ya utunzaji wa mazingira ikiwemo mistu.

Naibu Waziri huyo aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Allan Kijazi ambapo alimtembeza sehemu zote za Taasisi zilizoshiriki maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment