Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Vikundi vya wachimbaji wa wadogo wa mgodi wa Nyalilongo kushoto kwake pamoja na viongozi wa Wilaya ya Shinyinga walioko kulia kwake mara baada ya kukabidhi leseni za uchimbaji madini kwa vikundi tisa vya mgodi huo jana.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akikabidhi Leseni kwa Bi. Afsa Yusuphu Mwenyekiti wa kikundi cha Jipemoyo wakati wa zoezi la utoaji leseni kwa vikundi vya wachimabaji wadogo wa Kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo Wilaya ya Shinyanga jana

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiongea na wananchi wa mgodi wa Nyalilongo ulioko   Wilaya ya Shinyinga  jana kabla ya kukabidhi  leseni za wachimbaji  madini ya dhahabu kwa vikundi tisa vya mgodi huo jana.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko akiongea na wananchi wa mgodi wa Nyalilongo ulioko   Wilaya ya Shinyinga  jana kabla ya kukabidhi  leseni za wachimbaji  madini ya dhahabu kwa vikundi tisa vya mgodi huo jana. 

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philimon Sengati amemaliza mgogoro wa muda mrefu uliokuwa unawakabili wachimbaji wadogo wa mgodi mdogo wa Nyaligongo baada ya kukabidhi leseni tisa kwa vikundi tisa vya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wa mgodi huo mkoani Shinyanga.

Mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu ulioko katika Kijiji cha Nayaligongo Kata ya Mwakitolyo Mkoani Shinyanga sasa umefikia tamati baada ya Viongozi wa Vikundi tisa vya wachimbaji hao kupatiwa leseni rasmi za kuendelea na shughuli zao bila kusumbuliwa na baadhi ya wetu ambao wamekuwa wakishinikiza kuwahamishia sehemu nyingine.

Ni mgogoro huo uliofukuta kwa kipindi kirefu uliosababisha serikali Mkoani Shinyanga kuingilia kati na kuwarudisha katika maeneo yao na kuviwezesha vikundi hivyo kupata leseni za maeneo hayo ambazo zimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga DKT. Philemon Sengati.

Akiongea na wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyaligongo ambapo ndipo uliko mgodi huo Dkt. Sengati amesema serikali itaendelea kuwaunga mkono na kuwajengea mazingira mazuri ya utendaji kazi wao ili waendelee kufurahia maisha yao hapa Nchini.

Aidha Dkt. Sengati aliongeza kuwa hatua yake hiyo haitaishia kwa wachimbaji wadogo tu bali pia wale kiwango cha kati na cha juu na kuwataka wachimbaji kuendelea kukua ili waendelea kuchangia katika maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.

Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Wachimbaji wadogo katika kitalu namba kumi na tano Bw. Amrisaid Mlendi ameviambia vyombo vya habari baada ya kukabidhiwa leseni kuwa wameangaika kwa kipindi cha miezi sita kushughulikia mgogoro wao huku akiitaja Ofisi ya Kata kuhusika na mpango ambao ulikuwa unatekelezwa chini kwa chini.

Bw. Mlendi aliongeza kuwa wachimbaji wadogowadogo wako tayari kushirikiana na Serikali katika suala zima la ulipaji kodi na tozo za serikali na kutaka viongozi wa Serikali katika ngazi ya kata kuwa wawazi katika kushughulikia jambo hilo.

Wakati huo huo Bi.Afsa Yusuph mkazi wa Kata ya Mwakitolyo Wilaya Shinyanga alisema kufuatia zoezi la utoaji leseni kwa vikundi hivyo kukamilika sasa wananchi wamekuwa na uhakika na kazi zao kwani baadhi yao walishanza kuuza viwanja kwa hofu kuwa uenda wangefukuzwa katika maeneo yao.

‘’Tumepambania eneo hili kwa muda mrefu tangu tulipokabidhiwa hili eneo na Mhe. Rais   lakini hapa katikati watu walijitokeza na kutopola maeneo yetu lakini sasa tutafanya shughuli zetu bila wasiwasi’’. Alisisistiza Bi. Afsa.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko alisema baada ya kupata taarifa kutoka kwa viongozi wa vitalu vya madini alifika mgodini hapo na kusitisha zoezi la kuwahamisha katika maeneo yao ambayo wanayatambua na kuwataka kuendelea na kazi kama kama kawaida na sasa ni furaha yake kuona wamepatiwa leseni.

Bi. Mboneko katika hatua nyingine aliwataka wachimabaji hao kuchangia ujenzi wa zahanati ya kijiji na ujenzi wa zahanati hiyo unaenda vizuri na kuongeza kuwa zahanati hiyo itachangia zaidi katika huduma za mama na mtoto kwani kiwango cha akina mama kujifungua kiko juu katika jamii hiyo. 

Mkoa wa Shinyanga ni Mkoa wenye utajili mkubwa wa madini ya dhahabu ambayo madini hayo yanachimbwa na migodi mikubwa kama Twiga Barrick Gold Mines na ile midogo inayopatikana takribani katika Wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga.

 

Share To:

Post A Comment: