Afisa Masoko wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  kutoka Makao Makuu, Bi Jennifer Mgendi,  akizungumza  na Wananchi wa Kijiji cha Chibumagwa katika zoezi la utoaji wa elimu ya uhamasishaji  kuhusu utaratibu wa kuunganishiwa umeme kwa Bei ya Sh.27,000/= tu, wilayani Manyoni mkoani Singida jana.
Mwananchi wa Kijiji cha Chibumagwa, akitoa shukurani kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na REA kwa kuwafikishia umeme katika Kijiji hicho.
 Uhamasishaj ukiendelea.


Na Mwandishi Wetu,  Singida.


SHIRIKA  la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utaratibu wa kuunganishiwa umeme kwa Bei ya Sh.27,000/= tu.

Akizungumza jana katika zoezi hilo la utoaji wa elimu hiyo  wilayani Manyoni, Afisa Masoko wa Shirika hilo kutoka Makao Makuu,Bi Jennifer Mgendi alisema uhamasishaji huo unafanyika mkoa mzima wa Singida na wilaya zake zote.

"Uhamasishaji huu tunaufanya mkoa mzima na wilaya zake zote lengo ni kuwaelimisha wananchi ambao ndio wateja wetu wauelewe na wawatumia   wakandarasi waliosajiliwa ili waweze kuwafungia umeme kwenye nyumba  zao," alisema Mgendi.

Aidha Mgendi alisema kuwa kwa wale wenye nyumba zenye ukubwa mdogo watumie kifaa cha Umeta au Umeme Tayari  ili wapunguze gharama za kusuka nyaya kwenye nyumba zao.

Zoezi hilo la Uhamasishaji Mradi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)  Awamu ya Tatu, mzunguko wa Kwanza na Mradi Jazilizi unaoendelea mkoani hapa unafanywa na  Afisa Masoko huyo kutoka Tanesco makao makuu, Bi Jennifer Mgendi kwa kushirikiana na Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa  Tanesco Mkoa wa Singida, Bi  Witness Msumba.

Share To:

Post A Comment: