Nembo ya Next Room Singida
Muonekano wa moja ya Kaunta zake za ndani.
Muonekano wa baadhi ya viti ndani ya Restaurant hiyo.

Muonekano wa baadhi ya viti ndani ya Restaurant hiyo.
Mandhari ya kuvutia nje ya Restaurant hiyo.

Mandhari ya kuvutia nje ya Restaurant hiyo.



UNAPOPITA kila mahali kwa sasa ndani ya Manispaa ya Singida stori kubwa ya kimjini mjini ni juu ya uzinduzi utakaofanyika kesho wa RESTAURANT ya kisasa na yenye hadhi ya kipekee mkoani Singida maarufu "NEXT ROOM."  

Sio rahisi kupotea kiwanja hicho KIPYA kipo mjini kabisa nyuma ya Ofisi za Tanesco za Mkoa Mtaa wa Ipembe ni njiani kabisa, wanaotoka njia ya Jineri ukikunja tu kona ya Benki ya NBC kuingia sokoni unakutana na 'Next Room'. 

"Restaurant na Baa" hiyo ambayo wadau wengi wamekuwa wakiisubiri kwa muda mrefu sasa uzinduzi wake ni kesho Jumamosi, lakini mpaka muda huu ninapoandika ishu hii tayari kuna watu wameshajisajili na wapo counter pale site wanapasha. 

Tofauti na maeneo mengine, hawa jamaa 'Next Room' wamejipanga vilivyo sana kwenye masuala yote ya vyakula kuanzia breakfast lunch na dinner, jamaa wameamua kuajiri mashefu wale wanaotengenezaga misosi ya hotel za Nyota Tano, full kufunika!  

Ishu ya VINYWAJI ndio kabisaa usipime! vyote vyote vipo na mdau wakati anakula na kunywa atasindikizwa na SCREEN kubwa sana ambazo zimetapakaa kila mahali kuwanasa vizuri wale wapenzi Liverpool, Manchester United, Arsenal, Wekundu na sisi wa njanooo. 

Kiukweli pako fresh! Mandhari yake imetulia kama unavyoona kwenye picha hapo chini na unaruhusiwa hata kutoka kifamilia mana hakuna mbwembwe nyiiingi sana za mziki wa juu hapana! kuna mziki wa kiwango kiasi chake, na uzinduzi wa kesho utasindikizwa na 'Live Band kutoka pande za Kigoma.' 

Share To:

Post A Comment: