Na,Jusline Marco;Arusha


Asasi ya kilele ya sekta binafsi inayojihususha na kuendeleza tasnia ya horticulture nchini [TAHA] imezindua kongani la zao la Parachichi kanda ya Kaskazini katika kijiji cha Gyani(Njani)  kilichopo katika kata ya Nkoaranga halmashauri ya Meru mkoani Arusha kwa kuhamasisha uwekezaji katika zao hilo kutokana na fursa kubwa masoko iliyopo katika soko la kimatifa.


Akizundua Kongani hilo  Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha Agney Chitukuro amesema kama serikali ya mkoa kupitia halmashauri zake watashirikiana Taasisi hiyo kuhakikisha uwekezaji wa zao hilo unafanikiwa kwa asilimia kubwa ambapo amefurahishwa na uboreshwaji wa viwango vya zao la parachichi yatakayozalishwa vitakidhi viwango vya kimataifa.


"Fursa tunayo na huu ni mwanzo au mwendelezo wa kazi nzuri inayofanyika,tukishakuwa na uhakika wa soko na uhakika wa taasisi kama TAHA ambao wao wataweza kutuhakikishia kwamba mazao haya yatasimamiwa na fedha mtapata hiloni jambo la shuishukuru taasisi hiyo."Alisema Chitukuro


Alisema tasnia ya horticulture imetoa ajira kwa akina mama wengi na vijana na ni fahari ya serikali kuoa kuwa pato litokanalo na zao la parachichi linapanda kila mwaka ambapo aliwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo soki la uhakika katika nchi za bara la ulaya lipo ambapo katika kipindi cha miaka 3 mfululizo uzalishaji wa zao hilo jmeongezeka kutoka tani elfu 20 kwa mwaka 2015 hadi kufikia tani laki moja na elfu tisini kwa mwaka 2018.


Chitukuro alisema kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa zao hilo mauzo ya parachichi nje ya nchi yameongezeka kutoka yani elfu 3279 mwaka 2015 hadi kufikia tani elfu 9 ambapo tani hizo hazitoshi kukidhi mahitaji ya watumiaji wa zao hilo ambapo amesema hiyo ni fursa pekee katika wilaya ya Arumeru kwa kujikita kwenye uzalishaji wa zao la parachichi kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya kilimo hapa nchini.


Awali akiongea katika uzinduzi wa kongani hilo mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Dkt.Jacqline Mkindi alisema kuwa kilimo cha horticulture katika sekta ya kilimo kinachangia kwa kiasi kikubwa kujenga uchumi wa nchi sambamba na kutoa ajira kwa vijana katila masuala ya afya na lishe.


Aliongeza kuwa Kongani hilo limewaunganisha wakulima wadogo takri ani 200 wakiwemo wanaume na wanawake huku idadi kubwa ikiwa ni vijana ambapo tayari wakulima hao wamesha andaa maeneo ya uzalishaji wa zao hilo zaidi ya hekari 250 kwa msaada na ushirikiano wa taasisi ya TAHA pamoja na wataalamu kwaajili ya uzalishaji wa zao hilo.


Mkindi alisema kuwa wakulima hao wapo tayari kuwekeza kwenye kilimo cha zao hilo ambapo katika umoja wao wameweza kununua miche 500 kwa ajili ya kuanza kupanda kwenye kongani hilo ambapo kutokana na muitikio huo taasisi ya TAHA itaendelea kuhamasisha kwa kuendelea kutoa miche mingine kwa ajili ya kuendelea kuotesha katika kongani hilo.


"TAHA vilevile tutaendelea kuwajengea uwezo kwa kuhakikisha kwamba kuna kitalu cha miche ya maparachichi  kinachoendeshwa kibiashara ambacho kitakuwa kinazalisha miche yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko la parachichi na vilevile inayokidhi mahitaji ya idadi ya wakulima watakaokuwa tayari kuendelea kwenye zao hili la parachichi katika eneo hili."alisema Mkindi


Akitoa takeimu za zao hilo,Mkindi alisema mwaka uliopita uzalishaji wa zao hilo ulikuwa ni tani 39,000 huku uuzaji nje ya nchi ukiwa ni tani 8500 hadi 9000 ambayo iliingiza dola za kimarekani milioni 30 na kwa miaka mitatu ijayo kutokana na uwekezaji  wa zao hilo wanatarajiwa kuingiza zaidi ya bilioni 22 kutokana na uhitaji mkubwa uliopo katika soko la kimataifa.


Alifafanua kuwa katika shamba la hekari moja inaweza kuoteshwa miti  120 na gharama ya kuwekeza ni shilingi milioni 1.1 huku gharama ya kuhudumia shamba ikiwa sio zaidi ya shilingi laki tano ambapo TAHA wanaendelea kuwajengea uwezo wakulima juu ya zao hilo pamoja na kuhakikisha kuwa wanazalisha mazao yenye ubora unaohitajika katika soko la kimataifa.


Alieleza kuwa zao hilo lina fursa nyingi ikiwemo kutunza mazingira, ni tunda pia  hukamuliwa mafuta pamoja na kokwa lake kutengenezewa bidhaa za kutunza ngozi hivyo ifike mahali wakulima wawekeze katika zao hilo kwa wingi kwani linachangia katika ukuaji wa uchumi.


Baadhi ya wanakikundi wa kongani hilo akiwemo Moses Kitosio alisema kuwa baada ya TAHA kuwaeleza juu ya fursa zilizopo katika zao la Parachichi wamechukua sehemu kubwa ya mashamba yao kubadili mazao waliyokuwa wakiyalimakama zao la kahawa ambalo pia walilirithi kutoka kwa wazazi wao hivyo wanatarajia kunufaika kwa asilimia 100.


Kwa upande wake Mkulima Esta Mungure alieleza kuwa wamekuwa na miti ya parachichi ya kienyeji lakini pia haikuwa kwaajili ya biashara  hivyo kupitia kongani hilo la zao la parachichi wataweza kulima kilimo biashara ambayo uzalishaji wake ni mkubwa na utawainua kiuchumi.


Naye diwani wa Kata hiyo ya Gyani,Esau Skawa alisema wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwafikishia fursa hiyo ya kilimo cha kisasa cha zao la parachichi ambapo wanaamini kuwa watakachokipata ni mbadala wa kitu ambacho walikuwa wakitegemea skku zilizopita ambapo uchumi wao utainuka kupitia zao hilo.


Duwani wa Kata ya Songoro ..alisema kuwa wananchi wa maeneo hayo hawana budi kuipokea fursa hiyo ambayo ni mbadala kwani kilimo cha zao hilo kitawakomboa kiuchumi ambapo alisema kama madiwa wa kata hizo pacha watashirikia kuhakikisha wananchi wao wanalima zao hilo kwa wingi na hatimaye kuwainua kiuchumi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: