U


TAASISI yakuzuia na kupambana na rushwa Mkoani Dodoma(TAKUKURU)inamshikilia Luka Nkini mwenye umri wa miaka 38Mkazi wa Airport Dodoma kwa tuhuma  za kujifanya mganga wa kienyeji huku akiwataka baadhi ya wakina mama kingono kama sharti la kuwasaidia ambapo amejipatia kiasi cha Sh.Milioni 100 na tano na viwanja viwili.


Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkuu wa TAKUKURU  Mkoa wa Dodoma,Sostheness Kibwengo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utendaji wao wa kazi  kwa robo ya Januari  hadi mwezi Machi Mwaka huu.


 


Kibwengo amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo  ametenda kosa hilo kinyume na Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura namba 329 marejeo ya mwaka 2019.




Aidha amewataja wahalifu wengine ambao walikuwa wakishirikiana na Mtuhumiwa Nkini kuwa ni  Hussein Mvungi(44)mkazi wa Himo Mkoani Kilimanjaro ambaye nae ameshakamatwa na amekiri tuhuma dhidi yake pamoja na Bw. John Gabriel Munuo mkazi wa Sanyajuu Siha huku akimtaka Bwana Munuo kuripoti mara moja kwenye  Ofisi za Takukuru ambazo zipo karibu naye kabla ya rungu la Takukuru halijamfikia.


 


Katika hatua nyingine Kibwengo amesema kuwa  wameweza kuokoa zaidi ya Shilingi milioni900 pamoja na Nyumba moja  na kiwanja kimoja ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha sh Milioni 214,182,548 ni fedha ambazo zilikuwa haziwasilishwi NSSF na waajiri.




Hata hivyo Mkuu huyo wa Takukuru ametoa wito kwa wanachi kuwa makini na watu ambao ni matapeli kwani wamekuwa wakijifanya ni Maafisa wa Takukuru wa Mkoa kwakuwapigia simu na kuwataka kwenda  Dodoma au kuwatumia fedha na kwamba huo sio utendaji wa TAKUKURU hivyo wasihadaike bali watoe taarifa kwenye ofisi za Takukuru.


 


Share To:

msumbanews

Post A Comment: