Mbunge wa Singida Magharibi, Elibarick Kingu


 Wananchi wa Kijiji cha Kipunda Kata ya Mtunduru wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wao Elibariki Kingu baada ya kukagua mradi ya maendeleo yenye thamani ya sh.milioni 800.


Mkutano ukiendelea.
Viongozi wakijitambulisha kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
 



Na Dotto Mwaibale, Singida


MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibarick Kingu amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kipunda kata ya Mtunduru hivi karibuni alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi ya maendeleo aliyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

"Namshukuru mwenyezi Mungu na Serikali ya awamu sita inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan kwani miradi yote niliyokuwa nimeahidi imeanza kutekelezwa." alisema Kingu.

Kingu alitaja mradi ulioanza kutekelezwa ni wa zaidi ya milioni 800 ambao unatekelezwa kwa ujenzi wa Zahati,Vyoo na vyumba viwili vya madarasa pamoja na nyumba mbili za wauguzi.

Alitaja miradi mingine inayotekelezwa kupitia fedha hizo ni uchimbaji wa visima vya maji katika vitongoji vyote sita vya kata hiyo na kuwa mapema wiki ijayo wataanza ujenzi wa barabara ya Kipunda inayojengwa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Universal.

"Kwa hatua hii tumemaliza rasmi ahadi tulizozitaoa wakati wa kampeni." alisema Kingu.

Katika hatua nyingine Kingu aliwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa ushirikiano mkubwa wanaouonesha katika shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo ambapo alitoa ahadi ya kuangamiza ndege aina ya Selengwa wanaoharibu mazao ifikapo mwezi Julai.

Share To:

Post A Comment: