Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum (kulia) akiwaelezea Maafisa kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) namna uzalishaji wa juisi na soda za Jambo unavyofanyika katika Kampuni ya Jambo Group Company Limited Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde 
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Centre - TIC) Kanda ya Ziwa Pendo Gondwe ametembelea na kujionea shughuli za uzalishaji zinazofanywa katika Kampuni ya Jambo Group Company Limited ya Mjini Shinyanga na kueleza kuridhishwa na maendeleo makubwa yaliyofikiwa na Kampuni hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya nchi.

Meneja wa TIC Kanda ya Ziwa, Pendo Gondwe amefanya ziara hiyo leo Jumamosi Aprili 17,2021 akiwa ameambatana na Meneja wa Sheria wa Kituo cha Uwekezaji Godfrey Kilolo na Afisa Uhamasishaji na Huduma kwa Wawekezaji Kanda ya Kaskazini, Gaspar Tembo.

Akizungumza baada ya kujionea shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo Juisi, Soda,Maji,Biskuti,Mikate, Ice Cream,asali na kiwanda cha kusindika matunda, Gondwe amesema amefurahi sana kuona maendeleo makubwa yaliyofikiwa katika Kampuni ya Jambo.

“TIC tumefurahi sana baada ya kutembelea kiwanda hiki cha Jambo na tumeona maendeleo makubwa, yale malengo yote ambayo walitupatia sisi TIC kutuambia kwamba watatekeleza wameyatekeleza kwa kipindi kifupi sana”,amesema Gondwe.

“Mwaka jana Mwezi Julai hadi Septemba tulisajili viwanda vitano vya jambo kikiwemo kiwanda cha kutengeneza Biskuti, Ice Cream,Pipi, kuchakata matunda na asali pamoja na mradi wa kuanzisha kituo cha Redio na Televisheni. Leo Mwezi Aprili mwaka 2021 hiyo miradi yote imeanzishwa mingine ipo kwenye hatua za mwisho na mingine iko kwenye majaribio”,ameeleza Gondwe.

Amebainisha kuwa TIC inashukuru na kupongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na Kampuni ya Jambo Group Company Limited pamoja na uongozi mzima wa Mkoa wa Shinyanga na wananchi kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika Kampuni hiyo.

“Ndani ya Kampuni ya Jambo Group Company Limited kuna viwanda zaidi ya 14 .Ukipita nje unaweza kuona ni eneo la kawaida lakini ndani kuna viwanda vya kisasa vyenye mitambo ya kisasa na viwango vya kimataifa, vipo Shinyanga katika eneo moja na wamewekeza pesa nyingi katika teknolojia”,amesema Gondwe.

“TIC kwa kweli tunawashukuru sana miradi ya Jambo kwa sababu ni miradi ya mfano iliyopo Kanda ya Ziwa na kwa nchi yetu. Miradi ya Jambo inatuweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kwamba sasa Tanzania pia tuzalisha bidhaa zinazoweza kutambulika na kuheshimika duniani kote”,ameongeza Gondwe.

Ameeleza kuwa mashine zilizopo katika Kampuni ya Jambo ni za kiwango cha kimataifa zinazozalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu akiongeza kuwa Kampuni ya Jambo imekuwa mlipa kodi mzuri na imekuwa ikitoa ajira nyingi kwa wananchi na imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya nchi.

Amesema pia Jambo imefanikiwa kusaidia sekta zingine ikiwemo ya sekta ya kilimo ambapo imefunga mashine ya kuchakata matunda yakiwemo maembe,nanasi,machungwa na nyanya ambapo wananunua kutoka wananchi na wameanzisha kiwanda cha kutengeneza asali ambayo pia wananunua kutoka kwa wananchi.

Aidha mara baada ya kutembelea viwanda vya Jambo,Gondwe amesema TIC imebaini kuwa Jambo inakabiliwa na changamoto ya kukatika kwa umeme ambayo inasababisha hasara kubwa kwenye kiwanda wakati wa uzalishaji wa bidhaa pindi hitilafu inapotokea wanapata hasara hivyo Jambo imeiomba TIC izungumze mamlaka zinazohusika ikiwemo TANESCO ili kuhakikisha tatizo hilo linakwisha.

Changamoto nyingine ni kodi kubwa kwenye bidhaa wanazoingiza nchini mfano wanaagiza malighafi na sukari kutoka nje ya nchi hali inayochangia kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.

Katika hatua nyingine Gondwe amesema kazi kubwa ya TIC ni kuhakikisha wanahudumia wawekezaji waliowekeza hapa Tanzania wakiwemo wazawa ama wageni kutoka nje ya nchi.

Kwa upande wake,mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum amewashukuru TIC kutembelea Kampuni ya Jambo akieleza kuwa ziara ya TIC ina manufaa kwa TIC na Jambo ambapo wamepata fursa ya kuonesha na kutangaza viwanda vya Jambo kupitia TIC.

Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum (kulia) akimuonesha moja ya mitambo katika Kiwanda cha Juisi Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Ziwa Pendo Gondwe (katikati) wakati akitembelea Kampuni ya Jambo Group Company Limited Mjini Shinyanga leo Jumamosi Aprili 17,2021. Wa pili kulia ni Meneja wa Sheria wa Kituo cha Uwekezaji Godfrey Kilolo. Picha zote na Kadama Malunde
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum (kulia) akiwaelezea Maafisa kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) namna uzalishaji wa maji unavyofanyika katika Kampuni ya Jambo Group Company Limited Mjini Shinyanga.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum (kulia) akiwawatembeza katika kiwanda cha Maji Maafisa kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika Kampuni ya Jambo Group Company Limited Mjini Shinyanga.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum akionesha maafisa kutoka TIC namna uzalishalishaji wa maji na juisi unavyofanyika katika Kampuni ya Jambo. 
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum akipiga picha na maafisa kutoka TIC ndani ya kiwanda cha Maji, Juisi na Soda
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited akiendelea na kazi ya kupanga vinywaji kiwandani
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Ziwa Pendo Gondwe akimpongeza mfanyakazi mwanamke wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited aliyekuwa anaendesha mtambo katika kiwanda cha Maji, Juisi na Soda
Meneja wa Sheria wa Kituo cha Uwekezaji Godfrey Kilolo akimwelezea jambo Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum (kulia). Katikati ni Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Ziwa Pendo Gondwe.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum akiwaonesha maafisa kutoka TIC matunda yaliyosindikwa tayari kwa kutengeneza Juisi
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum akiendelea kuelezea namna mitambo inavyofanya kazi kiwandani
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum akionesha Biskuti za Jambo kwa maafisa kutoka TIC katika kiwanda cha kutengenezea Biskuti za Jambo
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum akiwatembeza maafisa kutoka TIC sehemu ya kiwanda cha kutengenezea pipi
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Ziwa Pendo Gondwe akiangalia pipi za jambo
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Ziwa Pendo Gondwe na Meneja wa Sheria wa Kituo cha Uwekezaji Godfrey Kilolo (kushoto) wakiwa wameshikilia pipi za Jambo
Ziara ya kutembelea Kampuni ya Jambo ikiendelea
Picha ya kumbukumbu
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum akiwaonesha maafisa kutoka TIC Skonzi zinazotengenezwa katika Jambo Bakery

Maafisa kutoka TIC wakiondoka Jambo Bakery iliyopo katika Kampuni ya Jambo Group Company Limited
Maafisa kutoka TIC wakiangalia asali inayotengenezwa katika kiwanda cha asali katika Kampuni ya Jambo Group Company Limited
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Ziwa Pendo Gondwe akimweleza jambo Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum katika kiwanda cha asali. 
Maafisa kutoka TIC wakiondoka katika kiwanda cha Ice Cream
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Khamis Salum akiwa na maafisa kutoka TIC katika moja ya Studio za Jambo FM

Picha zote na Kadama Malunde 
Share To:

Post A Comment: