Na,Jusline Marco;Arusha


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Dkt.Faustine Ndugulile amekabidhi hati ya eneo la ujenzi wa jengo jipya la shirika la Umoja wa Afrika unaoshughulikia masuala ya Posta Afrika (PAPU)  baada ya kumalizika kwa mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 25.


Akikabidhi hati hiyo katika Makao Makuu ya Shirika la Posta Duniani Ndugulile ameipongeza wizara na mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) ambao walithubutu kuhakikisha katika zoezi hilo wanaingia ubia kati ya serikali pamoja na Umoja huo(PAPU).


Aidha ameipongeza  wizara ya ardhi,wizara ya katiba na sheria,wizara ya mawasiliano teknolojia na habari,serikali ya mkoa wa Arusha pamoja na jiji la Arusha kutumia muda mfupi kuhakikisha wanatatua mgogoro huo ambao ulidumu kwa muda mrefu.


Kwa upande wake Postamasta mkuu wa shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe  anaeleza kuwa katika siku 100 tangu kuanzishwa kwa wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari wameamua kubasilisha mfumo wa utoaji wa huduma kwa kuanzisha mfumo mpya wa posta mkononi.


Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo inasema kuwa jengo hilo litakuwa na ghorofa 16 ambalo lilianza takribani miaka miaka 30 iliyopita na litagharimu shilingi bilioni 33.6 bila vat huku fedha zilizotumika zikiwa ni bilioni 8.4 na kutarajiwa kukamilika tarehe 26 mwezi juni mwakani ambapo katika jengo hilo kutakuwa na ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kubeba watu 500 hadi 600 kwa wakati mmoja.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: