Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw.Imani Sichalwe akizungumza na wauzaji wa nyama za mafungu katika Machinjio ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea katika maeneo hayo kwaajili ya kuwaondoa. Wauzaji wa nyama kwa mafungu wakiwa wamewpanga nyama zao kwaajili ya mauzo ambapo ni kinyume na utaratibu uliowekwa kwa maana unahatarisha afya kwa mlaji nyama zinazouzwa kwa njia hizo.

Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw.Imani Sichalwe akiwaelekeza wauzaji mifuko kuwa haitakiwi kwa kubebea nyama kwa maana yakuwa mifuko mingi inakuwa na kemikali ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu. Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw.Imani Sichalwe akishuhudia uuzaji wa nyama kwa mafungu katika maeneo ya machinjio Vingunguti ambapo aliwaamuru kuondoka mara moja kwa maana uuzaji wa nyama kwa mafungu katika maeneo hayo ni hatari kwa afya ya mlaji.

(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)

*******************************

NA EMMANUEL MBATILO. DAR ES SALAAM

Bodi ya Nyama Tanzania imewataka wauzaji wa nyama kwa mafungu maeneo ya machinji Vingunguti kuacha mara moja kwa maana unaweza kuhatarisha afya ya mlaji wa nyama hizo kwani wauzaji hawafuati utaratibu wa uuzaji wanyama.

Akizungumza baada ya kutembelea maeneo hayo Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw. Imani Sichalwe amesema uuzaji wa nyama kwa mafungu kiholela unaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu kwa maana uuzaji wa nyama hizo uuzwa katika maeneo ya wazi ambayo ni hatari.

"Kuanzia sasa huu uuzaji usitishwe mara moja, mazingira haya ni hatarishi kuna magari yanapita ule moshi wa gari ni hatari pia kuna inzi wa chooni pamoja na inzi wanaotoka katika uchafu wanaweza kusababisha magonjwa kama kipindupindu". Amesema Bw.Sichalwe.

Aidha Bw.Sichwale amewataka wauzaji kwenda katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwaajili ya biashara hiyo lakini sio maeneo kama haya ya wazi.

"Hapa tunaona kinyesi na mikojo karibu sana na hapa mnapouzia hizi nyama kwani ninyi hamuoni kama ni hatari kwa afya, mlipuko kwa mangojwa ukitokea wakwanza kuathirika ni ninyi ambao hamfuati utaratibu hapa". Amesema.

Hata hivyo amesema kuwa dhumuni la Serikali sio kuwakataza watu kufanya biashara bali kuwashawishi wafanyabiashara kufanya biashara zao katika hali nzuri na kuzingatia afya kwa mlaji.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: