Mhandisi Mazingira kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Daniel Manase akizungumzia kuhusu kazi ya kurejesha Mto Lukosi katika njia yake asili, Ruaha Mbuyuni Mkoani Iringa.


 

Mtambo aina ya Excavator ukifanya kazi ya kuiinua tuta kwa kupanga mawe katika mto Lukosi, ili kuurejesha katika njia yake ya asili.

Picha ni Banio linalotumika kupitisha maji kutoka katika chanzo na  kupeleka katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Ruaha Mbuyuni
Picha inaonesha Muonekano wa Tuta, likiendelea kufanyiwa kazi katika mto Lukosi, Ruaha Mbuyuni

 

Na Mwandishi  Wetu,Ruaha Mbuyuni–Iringa

Ukarabati wa kingo za Mto Lukosi uliyopo katika Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, unayopeleka Maji yake katika mto Ruaha mkuu na kutumika katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Ruaha Mbuyuni, umekamilika baada yakusombwa na mafuriko makubwa yalitokea mwaka jana, yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika ukanda wa nyada za nyanda za juukusini.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa kazi hiyo Mhandishi Mazingira kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Daniel Manase alisema mafuriko hayo yaliyoharibu kingo yenye urefu wa takribani mita 180, yalisababisha kingo za mto kubomoka n ahivyo mto kuacha njia ya asili nakuanza kupita kwenye mkondo mpya uliojitokeza.


Aliongeza kwakusema kuwa Kuhama kwa mto kulipelekea banio la skimu ya Umwagiliaji Ruaha Mbuyuni kukosa maji na mazao yaliyokuwa shambani yalikauka, Mhandisi Manase Alisema, baada ya kufika katika eneo hilo nakuona hali halisi kazi kubwa ilikuwa nikutengeneza barabara ya muda kwanza ili kuweza kufika katika eneo liliko haribika kutokana na mazingira kutokuwa rafiki.

Alisema, Kazi ya ujenzi iliendelea kwa kujaza mawe na vifusi katika ujenzi wa tuta ili kulimmarisha.

“Pamoja na kwamba tulikuwa na vifaa vyetu, tulipata msaada wanyongeza ya eskaveta, kutoka kwa muwekezaji Kilimanjaro express anayefanya uwekezaji katika maeneo hayo, nakufanya kazi usiku na mchana karibia masaa 29, ili kuweza kuzunguka na kuziba gema maana maji yalikuwa yanakula gema.”Alibainisha.

“Tulizunguka kwa umbali wa kilometa 25 ili kuweza kubeba mawe na vifusi kuhakikisha kazi inakamilika, mwanzoni tulikuwa tunazunguka umbali wa kilomita tano kutokana na kwamba hali haikuwa nzuri ikabidi tuzunguke hizo kilomita 25.”Alisisitiza Mhandisi Manase.

Mhandisi Manase alisema, Kazi ya kupandisha tuta ilikuwa na changamoto ya mvua kutokana na kwamba vifaa vilikuwepo, magari yaliyokuwa yakikwama yalikwamuliwa.

Aliendelea kusema kuwa kwasasa kazi hiyo imekamilika na wananchi katika maeneo hayo wanaweza kuendelea na shughuli za kilimo katika skimu ya Ruaha mbuyuni kama kawaida kwani hali ya mazingira sasa imesharudi katika hali yake ya kawaida.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: