Takukuru Mkoa wa Songwe imewafikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa Songwe Mh.Hassan Makube ,aliekuwa fundi msanifu Wilaya  ya Mbozi Jumapili Mwashilindi na Mkurugenzi wa Kampuni Sahene Enterprises ltd h Samson Mwakyembe


Mwendesha mashtaka kutoka Takukuru Mkoa wa Songwe Simona David Mapunda amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Mh Hassan Husein Makube  kuwa washtakiwa wote wawili  wanashtakiwa  kwa makosa mawili katika kesi ya uhujumu uchumi namba 3 ya mwaka 2021, watuhumiwa wote wawili wametumia nyaraka za uongo kumdanganya  mwajiri wao ambae ni  Halmashauri ya Wilaya ya  Mbozi kinyume na kifungu cha 22 cha PCCA namba 11/2007.


Amesema walitumia nyaraka hizo kwa mwajiri wao wakitaka kuonesha kuwa maghala ya Iyula na Ilomba yamekarabatiwa kulingana na BOQ jambo ambalo sio kweli na walidhamiria kumdanganya mwajiri wao ambaye ni Halmashauri ya Mbozi.


Katika shitaka la pili washtakiwa wote wawili wanashtakiwa kwa kosa la kuisababishia serikali hasara ya shilingi Milioni 24,180000 kinyume na aya ya 10 (1) na kifungu cha 57 (1) na 60 (2)cha sheria uhujumu uchumi sura ya 200 mapitio ya 2002.


Washitaki wote wawili baada ya kusomea mashtaka yao Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Songwe, Mh Hassan Makube  alisema dhamana iko wazi kwao na walitimiza masharti ya dhamana hivyo wapo nje kwa dhamana mpaka tarehe 03.03.2021

Share To:

msumbanews

Post A Comment: