MKURUGENZI wa Agri Thamani ambaye Pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia NGOs Mh Neema Lugangira akigawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za Sekondari
WANAFUNZI wa kike wa shule za Sekondari wakifurahia kupokea mfuko wao uliojaa taulo za kike za kutosha mwaka mzima kwa kila mmoja
FUSO lililokuwa limejaa Taulo za kike za wanafunzi wa kike 1800 wa Bukoba Manispaa likiingia kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini likitokea Dar es Salaam
Mabox ya Taulo za kike ambazo zote zilikuwa zimeandikwa Jina la Shule ya Sekondari kwa Idadi Kamili ya Wanafunzi wa Kike
Hivi ndivyo kila mwanafunzi wa kike alivyoondoka uwanja wa Kaitaba na Furaha



Mkurugenzi wa Agri Thamani; Mhe Neema Lugangiea (Mb.) ambae pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira ametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi 1800 kutoka kwenye shule 16 za Manispaa ya Bukoba .

 

Ambapo kila mwanafunzi mmoja ataweza kutumia taulo alizopewa kwa kipindi cha mwaka mmoja katika zoezi ambalo iliyofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kwa Manispaa ya Bukoba jumla ya packet 25,200 za Taulo za Kike ziligawiwa kwa Wanafunzi wa Kike 1,800 kutoka Sekondari 16 za Kata zote 14 za Manispaa ya Bukoba.


Akizungumza wakati wa ugawaji wa taulo hizo katika zoezi ambalo liliratibiwa na Idara ya Elimu Sekondari Bukoba Manispaa na Afisa Elimu Taaluma Sekondari alishiriki zoezi zima.

 

Mhe Neema Lugangira amesema ameamua kufanya hivyo ili kuwasaidia wanafunzi hao kuweza kujihifadhi na kuweza kuendelea na masomo yao wakati wa  kipindi cha hedhi.

 

Alisema wanafunzi ambao watanufaika na msaada huo ni kuanzia kidato cha tatu hadi cha nne ambao kwa sasa wataondoka na adha ambayo walikuwa wakikumbana nao wakati wakiwe kwenye kipundi cha hedhi.

 

“Naamini msaada huo utakuwa na manufaa makubwa kwao kutokana na kwamba watatumia muda mwingi kusoma hata wakiwa kwenye kipindi chao cha hedhi kutokana na kuwa na taulo ambazo zitawasaidia” Alisema Mbunge huyo.

 

Akizungumzia kuhusu msaada huo wa Taulo za Kike, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Bukoba Mjini Emanuele Ebeneza alimshukuru Mbunge Neema kwa msaada wake wa taulo za wasichana ambao utakuwa chachu ya kupunguza utoro shuleni.

 

Alisema kupitia msaada huo wanafunzi wengi watajua namna ya kujihifadhi na kupunguza utoro shuleni kwa sababu ya kutokujisikia vizuri kwenye kipindi cha hedhi.

 

“Niseme tu kwamba licha ya kutoa msaada huo lakini pia Mbunge Neema anafundisha wanafunzi juu ya hedhi salama,  anawaandaa kisaikolojia kupita kwenye kipindi cha hedhi na hivyo kuwaondolea hofu na anawapa elimu ya lishe bora inayowasaidia waepukane na changamoto ya upungufu wa damu (anemia) ”Alisema Afisa Elimu Sekondari Bukoba Manispaa. 

 

Afisa Elimu Sekondari huyo alisema kwamba pia Mbunge Neema Lugangira anawafundisha usafi hatua ambayo inasaidia kupunguza utoro ambao ungetokana na wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo wakati wa mzunguko wa hedhi.

 

“Kama unavyojua mzunguko wa wasichana unatokea kila mwezi mara moja na wakati mwengine wakishindwa kuhudhuria masomo hivyo alilolifanya ni kitu cha muhimu sana sana kwa maana ya wanasichana “Alisema Ndg Ebeneza

 

Mmoja wa wanafunzi hao Alisema kwamba changamoto kubwa ni kubwa pale pedi zinapokuwa zimekwisha wanashindwa kuishi kwa amani kabisa wakati wakiwa wanaendelea na masomo

 

Naye mwanafunzi mwengine amesema wanashukuru kwa msaada huo kutokana na kwamba wakati mwengine wamekuwa wakikosa shule kutokana na kutokuwa na taulo za kujihifadhi wakati wakiwa kwenye kipindi cha hedhi.

 

Hata hivyo Avitha Faustini ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari  Hamugumbe alimshukuru Mbunge Neema kwa msaada huo ambao amewapatia ambao umekuwa ni faraja kubwa kwao na kuwaondolea changamoto walizokuwa wakikumbana nazo.

 

Alisema wamepata ujasiri wa kuendele na masomo kwani kabla ya kupata Taulo  hizo walikuwa wakitokewa na hali hiyo wanakuwa wanyonge na wakati mwengine hulazimika kurudi nyumbani na  kukosa masomo. Aliongezea kwamba sasa hivi hawana haja ya kuwaomba wazazi pesa ya kununua pedi.

Mwanafunzi mwingine alikiri kwamba wengi hawajawahi kuziona taulo za kike na alielezea njia ambazo wengi wao wanatumia ambazo kwakweli hata sisi tunashindwa kuziandika maana sio salama kabisa. Mwanafunzi huyu alionyesha furaha ya aina yake kuona kwamba wamekumbukwa na kuthaminiwa hata kama wao ni watoto wa kimaskini.

Mradi huo wa Taulo za Kike umeshawanufaisha  Watoto wa Kike katika mikoa ya Dodoma, Tabora, Pwani, Tanga, Kigoma, Mtwara na Kagera na mikoa inayofuata kwa awamu hii ya kwanza ni Ruvuma na Lindi

Mbunge Neema Lugangira alimalizia kwa kusema kwamba Jumla ya Wanafunzi wa Kike 5,500 nchini watakuwa wamenufika ifikapo mwezi Mei 2021 ambapo Taulo za Kike zote zimetengenezwa na Kiwanda cha Tanzania ambacho kinauzoefu wa zaidi ya miaka 40 kwenye eneo hili.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: