Na Lucas Myovela _ Arusha.

Maafisa Michezo, wa Halmashauri zote hapa Nchini wapo katika mpango mkakati wa kuungana kwa umoja wao, Lengo likiwa ni kpandisha taifa katika nyanja mbali mbali za kimichezo na kukuza vipaji vya watanzania katika michezo.

Hayo yamesemwa na Benson Maneno, Afisa Michezo wa Jiji la Arusha katika kikao na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi wa kwanini wao wamepanga kuungana.

"Lengo letu ni jema la kuungana maana maana sisi maafisa michezo wa majiji tulitaka kuanzisha umoja wetu lakini tukashauliana tutanue wigo na kuona tu ungane wote maafisa michezo wa Halmashauri Tanzania, kupitia sisi Maafisa Michezo ni rahisi sana kupata watanzania wenye vipaji ambao wanaweza kulitangaza Taifa letu katika michezo mbali mbali". Amesema Benson Maneno.

"Ikumbukwe pia sisi tunafanya kazi ngazi za Halmashauri na ndipo kuna chimbuko kubwa la vipaji vya watanzania na mara nyingi vipaji hivi hupotea, Katika kuongeza ufanisi wa Michezo kwa vijana tutaweza kupanua ajira nyingi za watanzania wenye vipaji vya Michezo na tutaisaidia Serikali kupata wanamichezo bora katika Taifa letu". Ameongeza Benson Maneno. 

Aidha Benson Maneno, ameeleza kuwa kupitia umoja huo wa Maafisa Michezo kitu cha kwanza wataweza kubadilisha uzoefu wa utendaji kazi katika Halmashauri zote na pia wataweza kuomba Serikali kuongeza babajeti walizo nazo katika Halmashauri ili kuweza kuisaidia serikali katika michezo.

"Hivi karibuni  mawaziri wetu walitoa maelekezo ya Halmashauri zote kusimamia michezo lwa dhati na vipaji mashuleni na katika hili ni rahisi sana umoja wetu tutakao uwanzisha hata kuchangia mawazo yetu katika wizara zetu zinazo husika na michezo pamoja na Tamisemi kwa kufanya hivyo itakuwa ni rahisi sana kwa ukuaji wa Michezo hapa Nchini". Amesema Benson Maneno.

"Natumaini umoja huu utaleta matokeo chanya katika Michezo na nimatumaini yanhu tutashilikina na vyama vyote vya michezo hapaNchini ili tuwe na vipaji vya kisasa kwa watanzania".  Aliongeza Benson Maneno.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: