Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekagua mradi wa ujenzi wa Chuo kipya cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) katika  Mkoa wa Kagera.


Profesa Ndalichako amefanya ukaguzi huo Januari 9, 2021 wakati wa ziara ya siku moja mkoani humo ambapo amesema ameridhishwa na utekelezaji wa  Mradi huo ambao umefikia asilimia 50.7 ili kukamilika na ubora wa majengo yanayojengwa katika eneo hilo.



Waziri Ndalichako amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha mradi huo unakamilika mapema ili ifikapo mwezi wa nane mwaka huu uwe umekamilika.


"Kukamilika kwa mradi huu kutafanya Serikali iendelee kutimiza azma ya kuhakikisha inatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wengi zaidi wa Kitanzania ili waweze kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa viwanda.


Naye Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi  nchini, Pancras Bujulu amemweleza Waziri Ndalichako kuwa utekelezaji wa ujenzi wa majengo umefikia asilimia 50.7 na kwamba majengo yote yamekamilika  yakisubiri kazi ya uezekaji paa huku kazi ya kusawazisha ardhi na mazingira ikiendelea.


Bujulu amesema ujenzi wa wa chuo hicho unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Watu China kwa gharama ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 22.

Share To:

Post A Comment: