NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.



Halmashauri ya Arusha imeeleza sababu za halmashauri hiyo  kutokufikia lengo la ukusanyaji wa mapato kota ya kwanza  kwa mwaka 2020 kama ilivyojiwekea  makisio ya zaidi ya Billioni 59 na millioni 188 na kufanikiwa kupata Billioni 21 na Millioni 837 kufika December 31,2020.


Sababu hizo zimetolewa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Saad Mtambule  wakati akisoma taarifa za mapato na matumizi kwa mwaka huo kwa baraza la madiwani alisema kilichofanya wasifikie asioimia 100 kota ya kwanza ni pamoja na kokosekana kwa ulipaji kodi wa hiari kwa wafanyabishara na kuyumba kwa bishara ya utalii.


Mtambule alifafanua kuwa walipa kodi mbalimbali wengi wanahitaji kusukumana nao kwani ulipa kodi wa hiari umekuwa ni shida lakini kama halmashauri wamejipanga wenyewe kama watendaji kutoka na kutembea kwa oamoja kuhakikisha kila anayepaswa kulipa analipa na kile anacholipa kiwe kile kinachostahili kupokea.


“Anayefanya biashara awe na leseni na alipe anachostahili na tumekutana na hizi changamoto, wakati mwingine tunapelekana polisi wengine mahakamani lakini ndo hivyo mapato hayana lele mama lazima twende,” Alisema Mkurugenzi huyo.


Alieleza kuw sehemu zingine wamekuea wakiondoa vitabu vya ukusanyaji mapato na kupeleka mashine kama ilivyoelekezwa na serikali kwamba kila chanzo cha mapato inakusanywa kwa kupitia mashine hizo.



Alisema changamoto nyingine ni kushuka kwa biashara ya utalii ambapo alieleza kuwa uchumi wa Arusha unategemea  sana utalii na utalii ukifa kwenye mahoteli biashara inaenda chini ambapo kwanzia mwezi wa pili 2020 na hii changamoto bado inaendelea idadi ya watalii iko chini.


“Watalii wanapokuja sisi ndio biashara nyingi zinachangamka  ushuru wa huduma tupata hapo na ushuru huo ni sehemu ya mapato kwahiyo tumekutana na changamoto hizi  lakini kuna jitihada mbalimbali  tunaendelea nazo kama watendaji na tunaamini kufikia mwezi wa nne, watano tutakuwa tumefikia lengo tulilojiwekea,”Alisema.


Alifafanua kuwa wamebuni vyanzo vingine ambavyo vitawasaidia kukusnya mapato mengine ambapo ni pamoja na ujenzi wa shuele ya mchepuo wa kingereza ambayo imeshaanza kupokea wanafunzi lakini pia wanafanya kazi ya urasimishaji kwenye kata ya Mlangarini kijiji cha Kiserian na hadi tarehe january 25,2021 kuna watu wenye viwanja zaidi ya 3000 vilivyotambuliwa.


“Viwanja hivi ukizidisha mara laki moja na elfu hamsini utaona unaweza ukaona ni zaidi ya millioni 400 ambazo tukizipata tukizikusanya zitatusaidia kuongeza kiasi ambacho hakipo lakini pia kuna maeneo ya Engorora,Laroi tutaenda na penyewe kufanya urasimishaji,"Alieleza.


Alifafanua kuwa wanaendelea kubuni vyanzo ambavyo viko kwenue maeneo yao ambapo ni pamoja na kuja na wazo la kuanzisha kituo cha Radio ambacho kitawasaidia kujitangaza na kuondoa changamoto ya wakazi wa halmashauri hiyo wa mita 200 kutoka jiji la Arusha kutokuifahamu halmashauri hiyo na kwenda kulipa mapato jiji.


“Wafanya biashara wengi waliopo eneo la mita 200 upande wa halmashauri yetu unashangaa hawaijui halmashauri yao wanaenda kukata leseni jiji na ukiwauliza wanakuwa hawaijui Arusha DC na ili tuweze kujitangaza tumeona tuanzishe radio yetu na tayari tumeshaanza kulifanyia kazi,”Alisema.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: