Na ANDREW CHALE, CHALINZE.


MBUNGE Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amewahimiza wananchi wa Kitongoji cha Kisogo, Kijiji cha Visezi Kata ya Vigwaza kuhakikisha wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali kuepeleka Maendeleo katika kata hiyo na halmashauri yao. 


Akiongea katika mkutano na wananchi ambao alifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Mkurugenzi wa Halmashauri na wataalamu mbalimbali, Mheshimiwa Mbunge aliwasihi wananchi hao kuendelea kutambua umuhimu ambao Serikali ya Dr. Magufuli inafanya kuhakikisha maendeleo yanawafikia wanyonge wa Tanzania. 


Katika mkutano huo Mbunge alitumia mkutano huo kuagiza mamlaka husika kuhakikisha wanawafanyia tathimini ya fidia wakazi zaidi ya 100 wa vitongoji Vinne walio ndani ya eneo la kilometa 2.5 za barabra inayoelekea kwenye mradi wa  bandari ya nchi kavu ya Kwala.


Mbunge Ridhiwani Kikwete ameyasema hayo wakati wa ziara maalum ya Mkuu  wa Wilaya ya Bagamoyo, ambapo pia alitumia nafasi ya mkutano huo Kuwaondoa hofu Wananchi hao, ambao awali walitoa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Wilaya juu ya mwekezaji ambaye ni Mamlaka ya bandari nchini (TPA) kusitisha kupima ardhi ya maeneo yao ambayo yameelezwa kuwa ndani ya mipaka ya Serikali, hali ambayo wameshindwa kuendelea kupima ili kuwalipa fidia wananchi.


"Ardhi hii haiami. Ardhi hii ipo tunahitaji mradi huu uendelee nawaomba sana tupishe katika maeneo ambayo umepita. Kisogo ipo, vigwaza ipo, Chalinze ipo hakuna kitakachoharibika". Aliwahakikishia Mbunge Ridhiwani Kikwete.


Aidha, amewataka viongozi wa Kitongoji na Wenyeviti wa Kijiji kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo;......,,"Kubwa zaidi katika mradi huu utakapopita, viongozi tathimini ifanyike kamakwamba mgogoro umekwisha ili tutakapokamilisha pale mgogoro utakapokwisha tusirudi nyuma na kuambiana mali zilizokuwa kwenye maeneo hayo.


Barabara hiyo inayojengwa yenye urefu wa KM 9, inaanzia Vigwaza Mizani hadi eneo la bandari ya Nchi kavu iliyopo  eneo la Kwala.

Share To:

Post A Comment: