Wednesday, 6 January 2021

NAIBU WAZIRI WA HABARI SANAA NA MICHEZO ABDALLAH ULEGA ATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA TAIFA

 


Naibu waziri wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wizara ya Habari Sanaa na michezo mh Abdallah ulega ametembelea kambi ya timu ya Taifa "Taifa stars" ambayo inajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya DRC KONGO baada ya hapo timu itaelekea  cameroo kujiandaa na mashindano ya CHAN,


Mara baada ya kuwasili katika kambi hiyo Naibu waziri Abdallah ulega aliongea na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo na kuwataka kujua thamani ya timu ya Taifa katika nchi yetu kwani watanzania wote wako pamoja nao katika kuipeperusha bendera ya nchi kupitia mpira wa miguu,


Pia Naibu waziri huyo aliwataka wachezaji hao kujituma na kupambana kwa Hali na Mali na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ili kupata matokeo mazuri na kuliletea heshima Taifa,


Benchi la ufundi pamoja na wachezaji hao walimhakikishia Mh Abdallah ulega kuwa wanatambua jitihada za serikali kupitia wizara ya michezo ambayo imekuwa  ikitoa ushirikiano mkubwa kwenye secta hiyo na kuahidi kufanya makubwa katika mashindano na kuliletea Taifa heshima


Itakumbukwa timu ya Taifa "Taifa stars" iko kambini toka tarehe 1 January Kwaajili ya kujiandaa na mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment