Friday, 1 January 2021

MDAU WA MAENDELEO MUDDY GORYO AKARIBISHA MWAKA MPYA KWA KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE UHITAJI MAALUM SHULE YA MITINDO

 NA MWANDISHI WETU


MDAU wa Maendeleo Wilaya ya Busega ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Joseph Goryo 'Muddy'  ametumia wasaa wa mwisho wa mwaka kuwatembelea na kutoa zawadi watoto wenye uhitaji maalum katika shule ya Msingi Mitindo iliyopo Misungwi, Mwanza.


Goryo ameeleza kufarijika kwake kwa kutumia wasaa huo wa kutembelea watoto hao ambapo pia mbali ya kupata nao chakula cha pamoja aliweza kugawa zawadi maalum ikiwemo nguo zitakazowasaidia shuleni hapo.


"Leo nimekula chakula cha mchana na watoto wanaolelewa shule ya Msingi Mitindo na pia nimewapatia zawadi ya nguo watoto. Hakika tuendelee kuwaombea na  wanahitaji msaada wako ewe mtanzania watembeleeni muwaone na mtabarikiwa" Alisema Goryo.


Aidha, Alitoa wito kwa wadau wengine kutumia walichobarikiwa na kukitoa kwa wenye uhitaji ilikuwafariji.


"Tunaingia mwaka mpya kwa upendo na amani. Tunahitaji kushukuru kwa kila jambo pia tutumie siku hii ya kuuaga mwaka na kuupokea mwaka mpya kwa kutoa kwa wahitaji maalum" alimalizia Goryo


Mwisho.

No comments:

Post a Comment