NA NAMNYAK KIVUYO, AARUSHA


Chuo cha uhasibu Arusha baada ya kusaini mkataba na chama cha mpira sasa kimeanza mkakati wa kuinua na kukuza riadha hapa nchini kwa kuazisha IAA marathon inayotarajiwa kufanyika mei mwaka huu. 


hayo yaliezwa na mkuu wa chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka wakati wa ufunguzi wa mbio fupi zilizopewa jina la IAA fun run zitakazo fanyika kila mwezi kwaajili ya maandalizi  kuelekea mbio ndefu za kilomita 21 na 47 mei 2021.


Profesa Sedoyeka alisema kuwa wameanza kukimbia kilometa saba na nusu ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wanafikia malengo yao ya muda mrefu ya kuwa na marathon.



Alisema lengo kubwa la kuanzisha IAA marathon kuinyanyua na kukuza vipaji vya kukimbia kwani Tanzania hivi karibuni imekuwa kama kivutio cha watu kufahamiana, kuwa na undugu lakini pia kushereheka zaidi ambapo wamatamani siku moja timu ya riadha ya taifa ije kuwa na makao yake katika chuo hicho.


"Arusha iko nyanja za juu maana yake ni maeneo mazuri kabisa ya kufanya mazoezi ya mbio ndefu kwahiyo tunategemea kwamba IAA marathon italeta upizani mkubwa sana katika marathon nyingine na sisi tumejipanga kuhakikisha kuwa wale wote tutakao waalika watawashindanisha na kutoa mabingwa ambao wataweka rekodi za kitaifa kwenye kilometa 21 na 47," Alisema Professa  Sedoyeka.


Alifafanua kuwa hivi karibuni walisaini mkataba na chama cha mpira Tanzania(TFF) kwajili ya kunyanyua mpira wa miguu ambapo walishaanzisha ufadhili wa mpira huo na kwasasa ni kwaajili ya kukimbia riadha. 



Alieleza kubwa zaidi ni kukitangaza chuo kwani ndio msingi mkubwa wa biashara ambapo wanapokuwa wamekikuza chuo watakuwa na mvuto zaidi kwa wateja na hiyo ni moja kati ya mikakati yao kwa kuja na shughuli za kitaifa ambazo zitaweza kuvutia watu.


Aliendelea kusema kuwa chuo hicho ni sehemu ya Arusha hivyo lengo lingine ni kukuza utalii wa ndani na nje  ambapo kwa kufanya maradhon hiyo wanatarajia kuwavutia watu kutoka maeneo mbali mbali ya ndani ya nchi na nje. 


Aidha kuhisiana na mazoezi Profesa Sedoyeka alisema kuwa  ni muhimu kukumbuka  ili mtu aweze kuwa na akili nzuri, awe ni mwanafunzi au mwalimu, uwezekufundisha au kujifudha mwili unanafasi kubwa sana kwani kwa kufanya mazoezi mtu anaweza kuondoa mawazo(stress).


"Pamoja na kuondoa stress lakini pia unajenga mwili kwa kuweka vizuri usawa wa sukari, chumvi na madini mengine yaliypo mwilini pamoja na kuchochea unywaji wa maji  ambo unapelekea kuweka misuli, na damu sawa pamoja na kwenda kuondoa yale magonjwa yasiyoambukizika kama sukari, moyo, msogo wa mawazo na mengine," Alisema


Alisema kuwa kuwa sasa hivi sera ya taifa ya afya inalenga kwenye magonjwa ambayo sio ya kuambukiza na yalikuwa yamesahaulika ambapo kwa watu wa tasnia yao ambao wanakaa sana na kutumia akili nyingi ndo wako hatarini hivyo kwa kuanzisha shughuli hizo za mazoezi watalinda rasilimali watu vizuri na kupelekea kuongeza ubunifu kwa manufaa ya chuo na taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihingosi alisema kuwa mazoezi ya poamoja waliofanya kwa kushirikiana na chuo cha uhasibu yatajenga ushirikiano mzuri kati ya wanafunzi, viongozi na wananchi ambapo anaamini kiwa katika ushirikiano na kufanya kazi pamoja lakini pia mazoezi ni afya.


"Sisi kama serikali tunayapongeza mazoezi haya na tumeyabariki na tutazidi kuja kila watakapoandaa kwani yanaleta mahusiano mazuri na nikichocheo kizuri cha uchumi,"Alisema Keenan.


Alisema kuwa wanapofahamiana wanaweza kufanya shunguli mbalimbali za aidha za kizalendo kama vile ujenzi wa madarasa biashara na mengine mengi

Share To:

msumbanews

Post A Comment: