Saturday, 9 January 2021

DKT PIMA AWATOA WAZAZI HOFU ASEMA WANAWAFUNZI WOTE WATARIPOTI SHULE.

 
NA . NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Mkurugenzi wa jiji la Arusha,Dkt John Pima amewataka wananchi wa halmashauri hiyo kutokuwa na wasiwasi  ya watoto wao kutosoma  kutokana na upungufu wa madarasa kwani wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma.Akizungumza  na Mwananchi digital,Dkt.Pima amesema  hadi kufikia januari 11,2021 shule zitakapofunguliwa wataanza  na utaratibu  wa kawaida wa kusoma kwa awamu na baada ya hapo watarudi katika utaratibu ya wao kuwa na madarasa kamili.


"Niseme tu kwamba wananchi wasiwe na wasiwasi  bali waandae sare shule pamoja na vifaa vya kusomea kama daftari,vitabu, kalamu na kwenda kuchukua famu za maelekezo ya kujiunga(join instruction)ili wajiandae kwa masomo yanayotarajiwa kuanza 11,januari mwaka huu,"alisema Mkurugenzi Pima.


Dkt. Pima alisema hadi kufikia wanafunzi kuanza masomo watakuwa wamemaliza  hatua ya kufunika majengo matatu yenye jumla ya madarasa 12 huku shule ya sekondari mkono,Kinana na Muriet wnamadarasa sita ambayo hadi sasa yapo katika hatua ya uwezekaji.

No comments:

Post a comment