Na Ahmed Mahmoud Arusha Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amewapa siku nne maafisa utumishi wilayani humo kuhakikisha wanatatua changamoto za waalimu wapatao 67 wanaodai malimbikizo ya fedha zao. Aidha amebainisha kuwa fedha hizo ni pamoja na malimbikizo ya kupandishwa madaraja mishahara na fedha za kustaafu ambazo wamekuwa wakisotea kwa muda mrefu sasa bila kupata majibu ya Stahiki zao na barua kutofikishwa wizara ya elimu. . Akizungumza na waalimu hao wastaafu Mh lengai ole sabaya amesema kwamba serikali imekuwa ikijitahidi kulipa madeni lakini maafisa watumishi hao wamekuwa wakiwazungusha waalimu hao kupata mafao yao kwa makusudi wakiacha kupeleka barua zao kwa Katibu mkuu wa elimu kuizinisha malipi yao Sabaya amefikia uamuzi huo Mara baada ya afisa utumishi Semati Lendina kukiri makosa yake ya kuacha kushughulikia barua za wastaafu hao na kumuomba radhi mkuu huyo wa Wilaya kwa kukiri kumekuwepo na uzembe juu ya utekelezaji wa madeni ya wastaafu hao. Wastaafu hao wapatao 67 wanadai kiasi cha shilingi milioni 170 fedha zao za kupandishwa madaraja na zingine zikiwa ni fedha za mishahara pamoja na nauli za kuhamishwa eneo moja la kazi kwenda kwingine jambo lilopelekea kupeleka malalamiko hayo kwa Mkuu wa Wilaya. Wameeleza kuwa kumekuwepo na madai kwa maafisa utumishi hao wamekuwa kikwazo katika kupata stahiki zao kutoka hazina jambo linalowapa kipindi kigumu katika maisha yao ya ustaafu Wakizungumzia malalamiko hayo mwalimu Eliamulia kisiri pamoja na Charles kimambo wamesema kwamba walistaafishwa kazi bila kupewa haki zao za msingi ikiwemo mishahara kabla ya kustaafu ikiwemo pamoja na malimbikizo ya kupandishwa madaraja pamoja na fedha za kustaafu Waalimu hao mbele ya mkuu wa Wilaya walionyesha barua zao mbalimbali ambazo wameandika wakidai stahiki zao bila mafanikio na zimekuwa zikiishia kwa maafisa utumishi bila kuwafikia mabosi wao ambao ni wizara ya elimu hususani mtendaji mkuu ambaye ni Katibu mkuu wa elimu Hata hivyo Mara baada ya maamuzi hayo mkuu wa Wilaya alimwagiza afisa utumishi huyo yeye na wenzake wapatao watatu kujitathimini ni kwanini wasiwekwe ndani kwa masaa kadhaa kwa uzembe ndipo aliwasamehe Mara baada ya kukiri makosa na kusema kwamba huu ni mwaka wa baraka asingependa kumwona mtumishi wa serikali anaanza mwaka vibaya Afisa utumishi huyo akizungumza kwa niaba ya wenzake Semati Lendina aliomba radhi kwa kusema mkuu wa Wilaya naomba niombe radhi kwani tumeshindwa kufanyakazi ya kuwasaidia barua za wastaafu kufika kwa Katibu mkuu na kuagiza kulipwaa madeni yao. Mwisho wa mjadala huo Mara baada ya mkuu wa Wilaya kusikiliza kero za waalimu wastaafu hao mbunge wa jimbo la hai Saashisha Mafuwe alisema wako tayari kusaidiana na mkuu wa Wilaya kwenda kwa pamoja ofisi ya Katibu mkuu wa elimu kuomba waalimu hao kupata stahiki zao kwani walitumikia vyema serikali kipindi cha utumishi wao. Mkuu wa Wilaya ameagiza hadi kufikia siku ya ijumaa saa nne asubuhi afisa utumishi awe amefikisha malalamiko ya waalimu hao wastaafu Ofisini kwake na baadae kufikisha kwa Katibu mkuu wa wizara ya elimu kuomba kufanyiwa kazi malipo hayo
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: