Na John Walter-Manyara


Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Manyara imemfungulia mashtaka ya jinai Dunga Othman Omar kwa kujipatia shilingi Milioni hamsini na nane na laki nne kwa njia za udanganyifu.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu aamesema kesi hiyo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu namba CC.1/2021 ipo mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi  Manyara Simon Kobelo.

Waendesha mashtaka wa Takukuru katika kesi hiyo ni wakili Evelyne Onditi na Martin Makani.

Hati ya wito kwa mshatakiwa imetolewa na mahakama ambapo Dunga anatakiwa kufika mahakamani hapo februari 23, 2021 bila kukosa.

Makungu amesema uchunguzi dhidi ya Dunga umekamilika na unaonyesha kwamba Dunga alipokea fedha hizo kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wakulima watatu wa mjini Katesh waliokuwa na uhitaji wa Matrekta ambapo kila mmoja kwa kiwango tofauti kama ilivyofafanuliwa kwenye hati ya mashtaka iliyofikishwa mahakamani.

Inaelezwa kuwa Dunga alijipatia fedha hizo mwaka 2016 kwa kuwashawishi wakulima hao wa wilayani Hanang' kwamba anatoa huduma ya kukopesha matrekta kupitia kampuni aliyokuwa ameianzisha ya Farm Green Imprements (T) Ltd ambayo wanapaswa kuidai ilishakufa.

Takukuru imesema kuwa vitendo vya namna hiyo hutafsiriwa kama utakatishaji wa fedha na kinyume cha (12)  (The anti money Laundering Act, 2006)  na wale watakaobainika kudhulumu watu kwa mtindo huo watawajibika kwa mujibu sheria hiyo ya utakatishaji fedha. 

Share To:

Post A Comment: