Wednesday, 2 December 2020

WAZIRI MKUU AWAONYA WATAALAMU WA UNUNUZI WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VIOVU

 


NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewaonya wataalamu wa ununuzi na ugavi wanaoendeleza vitendo vya viovu vya rushwa na upendeleo katika manunuzi  kwani serikali itaendelea kuwachukulia hatua wote watakaobainika kuwa na makosa.


Waziri mkuu aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa 11 wa wataalamu hao ambapo amesema kuwa serikali inatambua umuhimu wa wataalamu wa manunuzi katika utekelezaji wa mradi kikubwa ya mikakati inayoendelea hapa nchini  pamoja na kutambua kuwa wapo wataalamu ambao uwezo wao unatiliwa mashaka.


Alieleza kuwa utekelezaji wa miradi unategemea weledi wao, ambapo uzembe na ukosefu wa weledi katika kusimamia mgogoro wa ununuzi na ugavi unapelekea kukwamisha  utekelezaji wa miradi au kufanyika chini ya kiwango hivyo bodi na taasisi zingine zichukue hatua mahususi za kuwajengea uwezo wa kufanya kazi zao kwa weledi na uwajibikaji mkubwa.


Aidha ameagiza wataalamua hao kuanzia kujengewa uwezo kutoka ngazi ya taaluma vyuoni ili wajione kuwa nilazima wawe  watu safi, waaminifu na watakaoweza kutumika katika kuokoa matumizi makubwa ya fedha za manunuzi.Kwa upande wake Waziri wa fedha na mipango Dkt Philip Mpango alisema kuwa kwa kuwa wizara yake ndio ina jukumu la kuusimamia ununuzi na ugavi ataendelea kuhimarisha taaluma hiyo na kuongeza nguvu ya kupambana ya kupambana na vitendo vyote vinavyokidhana na  maadili ya kitaaluma kama wizara, ubadhilifu,  rushes na upendeleo.


"Pia naiagiza bodi ya PSPTB kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa wataalamu wanaokiuka maadili na kujihusisha na vitendo vinavyosababisha hasara kwa serikali,"Alisema Dkt Mpango. 


Aidha alisema kuwa hatua za kisheria ziendelee kuchukuliwa kwa waajiri wa sekta ya umma na binafsi ambao wanaendelea kuwaajiri na na kufanya kazi za ununuzi na ugavi na watumishi ambao hawajasajiliwa na PSPTB kama sheria inavyoelekeza.


Alifafanua kuwa wizara ya fedha na mipango inatarajia wataalamu wa ununuzi na ugavi wahakikishe katika maeneo yao ya kazi kuwa thamani ya manunuzi ya huduma na aidha inaendana na fedha iliyotumika, yasaidie kujenga uwezo wa wajasiriamali wa ndani, kukuza ubunifu wa wazalishaji, ulinde uendelevu wa kiuchumi,kijamii na mazingira pamoja na  kuwa kioo cha maadili na uwazi katika mnyoro wa ununuzi na ugavi.


Naye kaimu Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi Godfrey Mbanyi amesema kuwa wameandaa kongamano hilo kwa lengo la kuwakutanisha na kuwaleta pamoja wataalamu hao na wadau wengine ili waweze kujifunza, kujadili na kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa mnyororo wa ununuzi na ugavi kwenye maeneo yao ya kazi.


Hata hivyo mada kuu katika kongamano ni kufikia ubora wa juu katika usimamizi wa mnyororo wa ununuzi na ugavi ambapo madhaifu na changamoto zinazojitokeza katika michakato ya  manunuzi yatajadiliwa pamoja na kuwekwa kwa maazimio na mikakati ya ukaguzi wake.

No comments:

Post a Comment