Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika Dr. Tulia Ackson kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ametoa msaada wa mifuko 100 ya Cement katika Shule ya Sekondari Lupeta iliyopo kata ya Iyunga ili kuwezesha ukarabati wa baadhi ya madarasa katika shule hiyo.


Dr. Tulia amesema>>> “Leo tumekuja hapa kwa ajili ya kuleta mifuko 100 ya cement baada ya kusikia baadhi ya changamoto zilizopo hapa ikiwemo uchakavu wa madarasa hvivyo basi naamini kwa umoja wetu kama wananchi tukishirikiana kwa nguvu moja tutaweza kupunguza changamoto hizi”


“Tunatamani watoto wengi waliofaulu kuja hapa kwa msimu wa 2021, wapate elimu iliyo bora kama ambavyo Serikali yetu chini ya Rais Magufuli imeelekeza watoto wote wapate elimu iliyo nzuri tena bila malipo ya ada” -Dr. Tulia Ackson


“Sote tunafahamu kwamba kiu ya kila mzazi ni kutaka mtoto wake apate elimu na ufaulu mzuri, niwaombe Walimu mfanye kazi yenu kwa uaminifu ili tufikie malengo” -Dr. Tulia Ackson


“Hizi nafasi zetu za Uongozi zitachukuliwa baadae na hawa watoto wetu na sisi kama wazazi na walezi tutatamani viongozi wetu bora waje watokee hapa Lupeta. Walimu tunawategemea sana na niwaahidi tu kwamba tutarudi tena na kushirikiana katika maendeleo haya tuliyoanza nayo”-Dr. Tulia Ackson

Share To:

msumbanews

Post A Comment: