Friday, 4 December 2020

TCRA KUANZISHA KIWANDA CHA VIFAA VYA KIELETRONIC.

 


NA NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.


Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Muhandisi James Kilaba amesema kuwa kutokana na ongezeko kubwa la watumijia wa vifaa vya kieletroniki mamlaka hiyo kwa kushirikiana na serikali ya awaumu ya tano wapo katika  mchakato wa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza simu janja, mashine za kukatia risiti pamoja mashine za kutokea umeme.


Muhandisi Kilaba aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya umahiri kwa mafundi simu kanda ya Kaskazini ambapo alieleza kuwa mpaka sasa Tanzania ina watumishi wa simu janja zaidi ya million 45 na ili watumishi hao weweze kumudu gharama za ununuzi na utengenezaji pindi vinapoharibika tayari wanamtazamo wa kuanzisha kiwanda.


"Nchi imekuwa ikiookea vifaa vya kieletroniki kutoka nje lakini tutakapokuwa na kiwanda chetu Wenyewe itasaidia kurahisisha upatikanaji kwa bei nafuu, kupata spea kwa haraka pamoja na kuwa na fursa za ajira kwa mafundi simu," Alisema Muhandisi Kilaba.


Alifafanua kuwa vifaa vitakavyotengezwa katika kiwanda hicho vikitumika kwa muda vitaharibika na kuhitaji kutengeneza kama ilivyo katika vifaa vinavyotoka nje ndio maana wakala na mafunzo ya umahiri kwa mafundi simu ili kuboresha ujuzi na utendaji wao wa kazi.


"Tumefadhili mafunzo kwa mafundi 200 kila mkoa  kutoka kanda zote hivyo nawasihi mafundi muone mafunzo haya kama fursa ya kujiweka katika ushindani na pia kama ujasiriamali,"Alieleza.


Alieleza kuwa kupitia mafunzo hayo pia wataweza kuimarisha usalama wa vifaa vya kieletroniki kwani mafundi hao watafanya kazi kwa kuzingatia sheria ambapo watapata vyeti vya kuhitimu mafunzo pamoja na leseni au vitali vya kufanyia kazi.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta alisema ni vyema mafunzo hayo yakawa chachu ya kuleta mabadiliko katika jamii kwani wanapoelekea fundi ambaye hawatakuwa na ujuzi hataruhusiwa kufanya kazi hiyo.


"TCRA, DRT na VETa angalieni ni jinsi gani mtaweza kufanya mafunzo haya yakawa na viwango vya elimu kama vile astashada na stashahada na hii itasaidia sekta hii ya ufundi simu kuwa rasmi kama zilivyo taaluma nyingine," Alisema Kimanta.


Aidha aliwataka mafundi hao kujiunga katika vikundi vitakavyo wasaidia  kupata mikapo kwa lengo la kukuza na kuboresha kazi zao na kuweza kujenga uchumi wa nchi.Naye Mkurugenzi mkuu  wa vyuo vya ufundi(Veta) Tanzania Dkt Pancras Bujuru amesema  mafundi waliomba kufadhiliwa mafunzo hayo ni 417 lakini waliopata nafasi hiyo ni 200 hivyo mahitaji ya mafunzo hayo ni makubwa kwani watanzania zaidi ya 4700 wameonyesha uhitaji.


"Mafunzo haya yanalenga kuimarisha usalama kwani matumizi ya vifaa hivi kwa sasa ni zaidi ya asilimia 65 na hali hii inaonyesha kuwa uhitaji wa mafundi simu ni mkubwa," alisema Dkt Bajuru.


 Mwenyekiti wa umoja wa mafundi simu mkoa wa Arusha Nasiri Mshana alisema  tasnia hiyo ni umuhimu hasa wakati huu ambapo sayansi na teknolojia inakuwa kwa kasi hivyo TCRA iendelee kufadhili mafunzo ili kukidhi mahitaji.


"Ni lazima kuwa na mafundi wataalamu ma wenye weledi wa hali ya juu kutokana na umuhimu wa suala hilo katika nchi yetu hivi sasa ambapo mtu akiwa na simu janja anakuwa  sio na simu tuu bali ni vifaa cha kazi,"Alieleza.


Mkuu wa mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini Muhandisi Imelda Salum aliwasihi mafundi simu ambao bado hawajajiunga na umoja wao kuna haja ya kujiunga ikiwa ni pamoja na kuchukulia mafunzo hayo kama fursa ya kuboresha kazi zao na kama utambulisho wao kwa jamii kuwa wana ujuzi na weledi wa kutosha.

No comments:

Post a Comment