Mkurugenzi wa Taasisi ya ya Agri Thamani Foundation Neema Lugangira (MB) kushoto akisalimiana na Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (MB) Job Ndugai wakati wa hafa hiyo

Mhe Balozi wa China, Mhe Wang Ke kushoto akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi Shule ya Sekondari ya Ibwiga iliyopo Wilaya ya Kongwa katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya ya Agri Thamani Foundation Neema Lugangira (MB) ambayo  imezindua Mradi wa kutoa Msaada wa Taulo za kike kwa Wanafunzi wa Sekondari wa Kike.  

Mkurugenzi wa Taasisi ya ya Agri Thamani Foundation Neema Lugangira (MB) akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mhe Balozi wa China, Mhe Wang Ke akizungumza wakati wa halfa hiyo
Wanafunzi Shule ya Sekondari ya Ibwiga iliyopo Wilaya ya Kongwa wakiingia kwa shairi kabla ya kuanza makabidhiano hayo




TAASISI ya Agri Thamani Foundation iliyopo chini ya Neema Lugangira (MB) ambaye ni Mkurugenzi  imezindua Mradi wa kutoa Msaada wa Taulo za kike kwa Wanafunzi wa Sekondari wa Kike. 

Lengo la awali lilikuwa kufikia watoto wa kike 1,500 lakini sasa utafikia watoto wa kike 3,000 kutoka Mikoa 6; Dodoma, Tanga, Tabora, Kigoma, Kagera na Lindi. 


Mradi huu umezinduliwa kutoka Shule ya Sekondari ya Ibwiga iliyopo Wilaya ya Kongwa, Mkoa Dodoma. Jumla ya watoto wa kike 95 ambao mwakani 2021 wanaingia mwaka wa mitihani (Kidato cha Pili na Kidato cha Nne) wamepokea msaada wa Taulo za Kike za kuwatosha kwa kipindi cha mwaka mzima kila mmoja.
 
Hivyo, Agri Thamani inaamini kwa kufanya hivi watoto wa kike hawa hawatakosa shule na hatimae itachangia kuongeza ufaulu wao kwenye mitihani ya mwakani huku wakiwa na afya na usafi binafsi. 

Agri Thamani pia wametoa box lenye jumla ya packet 100 za taulo za kike kwa ajili ya kuwepo shuleni kukidhi mahitaji ya dharura ya mtoto wa kike.

Uzinduzi huu umehudhuriwa na Mhe Balozi wa China, Mhe Wang Ke ambao wanashirikiana na Agri Thamani katika Mradi huu.

Katika Hafla hii ya Uzinduzi, Mhe Neema Lugangira (Mb) aliwasilisha ombi kwa Mhe Balozi wa China, Mhe Wang Ke la kuanzisha Mradi wa Wanafunzi wa Kike wanaomaliza Kidato cha Sita kupata Ufadhili wa kwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China kwenye masomo ya Sayansi. 
 
Mhe Balozi hapa alikubali ombi hilo na kwa kuanzia mabinti 3 waliomaliza mwaka huu 2020 watachaguliwa kupata ufadhili huu na watatoka Wilaya ya Kongwa, Dodoma na Wilaya ya Bukoba Mjini Kagera. Mhe Neema Lugangira ataratibu zoezi hili kwa kushirikiana na Mamlaka za Wilaya husika.

Wanafunzi kwa umoja wao wametoa Shukurani kwa Mhe Neema Lugangira (Mb) kwa kuwajali wanafunzi wa kike. Mmoja wao kwa niaba ya wote atoa Shukurani hizo mbele ya wageni.

Awali akizungumza Mgeni rasmi Mhe Mbunge wa Jimbo la Kongwa ambae pia ni Mhe Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(MB), Mhe Job Ndugai alisema msaada huo wa taulo utakuwa chachu kwa wanafunzi wa kike kuweza kusoma bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ile

Alimshukuru Balozi huyo kwa kukubali ombi la mbunge Neema la kusaidia mabinti hao huku akieleza msaada huo unaweza kuchukuliwa kama kitu kidogo lakini ni mkubwa wenye thamani kubwa sana .

"Maana ni muhimu sana tuwasaidie watoto wa kike lakini nishukuru kwa shule ya Ibwaga kuchaguliwa kufanyika kwa uzinduzi huo huku akiliomba Shirika la Agri Thamani kuweka ofisi Kongwe ili jitihada na mashirikiano hayo yaendelee.

Naye kwa upande wake Balozi wa China nchini Mhe Wang Ke alihaidi kuendelea kushirikiana na Shirika la Agri Thamani na wataongeza ufadhili ili mradi wa Taulo za Kike ufikie mabinti wengi zaidi. huku wakikubali  ombi la Shirika hilo la Agri Thamani la "Scholarship" za Masomo vyuo vikuu China
 
 Mhe Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Suleiman Serera aliwapokea wageni na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama.






Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: