ADHA ya maji inayowakabili wananchi wa Kijiji cha Lukata Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya itafikia tamati baada ya serikali kutoa fedha zaidi ya shilingi milioni mia moja na kumi na tisa ili kukamilisha mradi huo

.



Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi alipotembelea vyanzo vitatu vya maji katika Halmashauri za Busokelo na Rungwe.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rungwe Antony Mwantona amesema Wilaya ya Rungwe ina vyanzo vingi vya maji hivyo haoni sababu za wananchi kukosa maji.


Anyosisye Njobelo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Busokelo na Mpoki Mwankuga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe wamesema ukosefu wa maji unachangiwa na wataalamu kutojituma kufanya kazi na kusubiri taarifa za kuletewa mezani.


Licha ya Wilaya ya Rungwe kuwa na vyanzo vingi vya maji lakini baadhi ya maeneo yanakosa maji kutokana na miundombinu yake kuchakaa au miradi kubuniwa vibaya.


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: