Wednesday, 30 December 2020

MH.UMMY AUNGANA NA WANANCHI WA TANGA KUMZIKA BABA ASKOFU ANTHONY BANZI

  


Mbunge wa Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu 29/12/2020 ameungana na mamia ya wakazi wa Tanga na nje ya Tanga kumzika Baba Askofu Hayati Antony Banzi katika kanisa la Mtakatifu Antony Wapadua Tanga Mjini. 


Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mhe Kasimu Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Akiongea katika mazishi hayo kwa niaba ya wanawake wote waliohudhuria mazishi hayo, Mh.Ummy amemuelezea Hayati Baba Anthony Banzi kama baba mwema, mwenye upendo, huruma na unyenyekevu kwa kila mtu. Na kuwa yeye ni mmoja wa wanufaika wa upendo wa Baba Askofu Banzi.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.


Imetolewa na:-Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Tanga Mjini

No comments:

Post a Comment