Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo amezindua kisima cha Maji eneo la Bihawana,Kata ya Mbabala ambacho kimefadhiliwa na Taasisi ya Pole Pole ya Alessandria,Italia kufuatia maombi yaliyowasilishwa kwa pamoja na Kanisa.


Mbunge Mavunde ameishukuru Taasisi ya Pole Pole ya Italia kwa msaada mkubwa wa kuhakikisha huduma ya Maji safi na Salama yanapatikana katika eneo hilo la Bihawana na kutumia fursa hiyo kuwataka wananchi wautunze mradi huo.


"Ninawaomba wananchi wote mhakikishe mnaulinda na kuutunza

Mradi huu ili uendelee kuleta manufaa kwa jamii kwa ujumla.Maji ni huduma muhimu sana kwa ustawi wa Maisha yetu na Afya zetu,nitaendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali kutatua changamoto zinazowakabili na nitahakikisha changamoto ya maji inakuwa historia kwenye kata yenu"Alisema Mavunde


Akizungumza katika Hafla hiyo,Makamu wa Askofu wa Jimbo Kuu Dodoma Padri Onesmo Wissi ameishukuru Taasisi ya Pole Pole kwa kugharamia mradi huo mkubwa wa Maji wenye gharama ya zaidi ya Tsh 60m na kuahidi kushirikiana na Mbunge Mavunde kutafuta wafadhili wengi zaidi wa kuja kusaidia kuboresha huduma za Kijamii ndani ya Jimbo la Dodoma Mjini.


Akishukuru kwa niaba ya wananchi,Diwani wa Kata ya Mbabala Mh Paskazia Mayalla ameahidi kupitia serikali ya mtaa kuulinda na kuutunza mradi huu wakishirikiana na Kanisa kwa kuwa ni wenye tija na manufaa kwa wananchi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: