1.    Profesa. Robinson Mdegela Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) akiwasilisha mada kuhusu tatizo la Usugu wa Vimelea kwenye dawa kwenye mkutano wa  37na Kongamano la Kisayansi la Chama cha wataaamu wa Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) jijiniArusha.

Mhadhiri kutoka Chuo cha Afya cha Muhimbili Profesa,  Japhet Killewo wakati akiwasilisha mada yake kuhusu mbinu ya afya moja katika kukabiliana na Magonjwa ya kuambukiza.

1.    Wajumbe wa Mkutano huo na washiriki wengine kutoka mikoa yote ya Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa.

  Wajumbe wa Mkutano huo na washiriki wengine kutoka mikoa yote ya Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa.
  Wajumbe wa Mkutano huo na washiriki wengine kutoka mikoa yote ya Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa.
  Wajumbe wa Mkutano huo na washiriki wengine kutoka mikoa yote ya Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa.


Na Calvin Gwabara, Arusha.


TATIZO  la Usugu wa vimelea kwa dawa ni kubwaduniani na linaweza kuzuiliwa kwa kutimiaushirikiano wa sekta mbalimbali (Afya Moja) kwakuwa ni tatizo la jamii nzima.

Hayo yamebainihswa na Profesa. Robinson Mdegela kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakati akiwasilisha mada kuhusutatizo la Usugu wa Vimelea kwenye dawakwenye mkutano wa  37 na Kongamano la Kisayansi la Chama cha wataaamu wa afya yajamii Tanzania TPHA jijini Arusha.

“Tatizo hili limeshafanyiwa tafiti nyingi sana namachapisho mengi sana yamechapishwayakizungumzia tatizo karibu kula chapisholakini wakati umefika sasa tuachanane nakulalamikia tatizo bali tutafute ufumbuzi watatizo sisi kama wataalamu kwa umoja wetu” alisisitiza Profesa Mdegela.

Alisema ili kupunguza na kumaliza tatizo hili nilazima elimu itolewe kwa jamii kujua tatizo iliwajiepushe na utumiaji wa dawa bila kufuataushauri wa wataalamu wa afya,kutomaliza dozina na hata mifugo yao kwakuwa tatizo hilolinaweza kupitia kwenye mazao ya mifugokama vile maziwa,Nyama na mayai.

Profesa Mdegela aliongeza kuwa uzalendounahitajika kwa wauzaji wa madawa yabinadamu na mifugo lakini pia kwa wafugajikwa kuzingatia kanuni za utoaji wa dawa nachanjo kwa mifugo yao kabla ya kuuza mazaoya mifugo hiyo.

“Kukosekana na fidia ya mifugo kwa mfugajialiyempatia mfugo wake dawa inayomhitajikutomchinja au kuuza maziwa au mayai yakendani ya muda Fulani baada ya kumpatia chanjoau dawa kunasababisha wafugaji kushindwakutupa mfano mayai,nyama na maziwa katikakipindi hicho na hivyo kuwauzia watu na mazaoyenye dawa kwa kuogopa hasara na hivyokuchangia kwenye tatizo hili la usugu wavimelea kwa dawa"alisisitiza Mdegela.

Mtafiti huyo kutoka SUA aliyebobea kwenyemasuala ya ufugaji na afya ya samaki hasaKambale aliongeza kuwa kuna haja ya kuongezawataalamu wa tiba ya wanyama nchini hasawale wenye stashahada na astashahadakwakuwa ndio wanaoweza kufanya kazi vijijinitofauti na wale wenye ngazi ya shahada nakuendelea kwakuwa hawakubali kukaa vijijiniambako ndiko kwenye mifigo mingiwanakimbilia mijini.

Aliendelea kueleza kuwa Tanzania kuna Shuleya kuzalisha wataalamu wa tiba ya afya moja tuambayo ipo SUA pekee wakati Ethiopia wanazo17 na kwaajili ya ngozi tu  na ndio kozi ambayoinakimbiliwa na kupendwa na wanafunzi wengiSUA kwani wakati inaanza ikiwa chini ya chuokikuu cha Dar es salaam ilikuwa na uwezo wakuchukua wanafunzi 25 lakini sasa zaidi yawanafunzi 200 wanaingia kila mwaka lakinichangamoto ni soko lao limebaki kwa sektabinafsi tu.

“Mataalamu wa mifugo wanapuunzwa kamaamabavyo jamii inapuuza mifugo yao maanaukimwambia mfugaji ampeleke mfano ngombewake mgonjwa kufanyiwa upasuaji mdogo wamoyo kwa ambao utagharimu labda laki sabawakati ngombe huyo anauzwa kwa laki tatumfugaji ataona bora akamchinje na hiiinapelekea watu kula nyama za mifugoinayoumwa maana ndio wafugaji wanaowauzasana wakiona ana tatizo badala ya kutibu” alifafanua Profesa Mdegela.

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Chuo  cha Afya cha Muhimbili Profesa Japhet Killewo kutoka wakati akiwasilisha mada yake kuhusumbinu ya afya moja alisema kuwa watu wengihawajui uwepo wa magonjwa hayo hatari yakuambukiza na wanajua hawaoni sababu yakuyatatua kwakuwa wananufaika na uwepo huo.

Alisema kuwa changamoto nyingine kuwa niuwepo wa wataalamu wachache wenye ujuzi wakutosha na hivyo kupendekeza dawati la afyamoja katika Ofisi ya Waziri Mkuu litafute nakutumia wanafunzi wa diploma na chetikuendesha kampeni mbalimbali za chanjo kwaniinasaidia wanafunzi kama mafunzo lakinikufanikisha vizuri kampeni za kutokomezamagonjwa hayo ya kuambukiza.

“Serikali isaidie kuelimisha jamii kupunguzamatumizi makubwa ya madawa bila kufuataushauri wa wataalamu ili kuondoa tatizo hili la usugu wa vimelea kwenye dawa na halmashaurikwakuwa ndizo zenye fedha zichangie fedhakwenye kampeni mbalimbali za chanjo kwenyebajeti zake za kila mwaka hii itasaidia sanakumaliza mfano kichaa cha mbwa namengine”alisistiza Prof. Killewo.

Mkutano huo wa  37 na Kongamano la Kisayansi la Chama cha wataaamu wa afya yajamii Tanzania PHA unakutanisha zaidi yawatafiti,Wataalamu wa afya,Mazingira,mifugo200 kutoka Mikoa yote nchini pamoja naWanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchinihususani Muhimbili,SUA,na vyuo vinginekuwapa nafasi ya kuwasilisha matokeo yao yautafiti wanaoufanya kama sehemu ya shule yao.

Share To:

Post A Comment: