Na Esther Macha,Mbeya


WAKUU wa Wilaya Mkoani Mbeya wamempongeza  Naibu Waziri wa maji Mhandisi , Maryprisca Mahundi (MB),kwa kuaminiwa na Rais magufuli  kwa  kumteua kwani utendaji wake kazi wanaujua vizuri.

Akizungumza wakati wa kikao cha kutoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza Mkuu wa Wilaya ya Rungwe ,Julius Charlya alisema kuwa kwenye familia ya wakuu wa wilaya wanajivunia uteuzi huo kwa Naibu Waziri.


Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa wana imani na Maryprisca kwani toka akiwa mkuu wa wilaya aliweza kufanya kazi yake vizuri hususan katika kusimamia suala la elimu katika wilaya ya Chunya.


“Niungane na wakuu wa wilaya wenzangu wa Mkoa wa mbeya kumpongeza Maryprisca yeye alikuwa katibu wangu mimi nilikuwa mwenyekiti katika familia ya wakuu wa wilaya tunajivunia  kwa mwezetu huyu  kuaminiwa na Mh Rais kuteuliwa nafasi hii muhimu tunajua uwezo wake kiutendaji atasaidia Mkoa wa Mbeya katika suala la maji “alisema Mkuu huyo wa wilaya.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chunya  Mayeka Saimon alisema kuwa kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya alikuwa anaungana na wakuu wa wilaya wenzake katika kumpongeza Naibu waziri wa maji kwa kuaminiwa na Rais Magufuli na kuamini kuwa changamoto za maji zilizopo katika maeneo mbali mbali mbali zitapatiwa ufumbuzi.


“Hata kuongoza  ufaulu kimkoa  wa matokeo ya mwaka huu ya darasa la saba ,naweza kujivunia pia maana mkuu wa wilaya mwenzangu aliyekuwepo Mandisi Maryprisca ndiye  aliyeweza kufanikisha haya na mimi nikapokea kwa kufuata nyayo zake alizoacha na ndizo zilizofanikisha aya yote tunasema asante Rais Magufuli “alisema Mayeka.


Naye Mbunge wa Jimbo la Rungwe ,Antony Mwantona alipongeza uteuzi huo kwa Naibu waziri tunategemea matatizo ya maji yataisha hasa kwa baadhi ya maeneo ya wilaya ya Rungwe na maeneo mengine ya mbeya yana changamoto kubwa ya maji .


“Tunategemea dada yetu sababu ni Naibu waziri wa maji matatizo ya maji kwa kiasi fulani yatapungua  au kuisha ukombozi utaanzia nyumbani mungu akusaidie sana katika utendaji wako “alisema Mbunge huyo.


Akitoa shukrani katika kikao hicho ,Naibu waziri wa maji (MB)Mhandisi Maryprisca Mahundi alisema kuwa waombane afya njema katika kufanikisha kazi za wananchi na kutatua changamoto za maji .


“nimshukuru rais kwa kuonyesa imani kubwa juu yangu aliweza kuniamini na kunipa wilaya ya chunya nilifanya kwa sehemu namna mungu alivyoniwezesha lakini bado hakufa moyo na kunipa nafasi hii tena, niweze kusaidia wizara ya maji na sasa tayari tupo kazini kuhakikisha kuwa matarajio ya mh Rais na watanzania kwa ujumla  kusogeza huduma ya maji yanakwenda kufanikiwa “alisema Mhandisi mahundi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: