Sunday, 6 December 2020

SEKTA YA KILIMO ITAENDELEA KUPEWA KIPAUMBELE- MAJALIWA

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Wazalishaji wa Mbogamboga na Matunda Tanzania (TAHA) Mhandisi Zebadiya Moshi,(kulia) wakati wa mkutano wa kanda wa uwekezaji katika sekta ya Mazao ya Bustani (Horticulture) uliyofanyika Disemba 5, 2020 kwenye Hoteli ya Hyat Regency, Jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungunza kwenye mkutano wa kanda wa uwekezaji katika sekta ya Mazao ya Bustani (Horticulture) uliyofanyika Disemba 5, 2020 katika Hoteli ya Hyat Regency, Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Aboubakar Kunenge akizungunza kwenye mkutano wa kanda wa uwekezaji katika sekta ya Mazao ya Bustani (Horticulture) uliyofanyika Disemba 5, 2020 kwenye Hoteli ya Hyat Regency, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Wazalishaji wa Mbogamboga na Matunda Tanzania (TAHA) Mhandisi Zebadiya Moshi akizungunza kwenye mkutano wa kanda wa uwekezaji katika sekta ya Mazao ya Bustani (Horticulture) uliyofanyika Disemba 5, 2020.
Mtendaji Mkuu wa  Asasi ya Mazao ya Bustani (TAHA) Dkt.Jacqueline Mkindi akizungunza kwenye mkutano wa kanda wa uwekezaji katika sekta ya Mazao ya Bustani (Horticulture) uliyofanyika Disemba 5, 2020.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha na pamoja na viongozi mbalimbali. (Picha na Emmaanuel Massaka, Michuzi TV.)


 WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kukipa kipaumbele kilimo cha mazao ya bustani kutokana na fursa nyingi zinazojitokeza kupitia mazao hayo yakiwemo matunda, mbogamboga, viungo, mizizi na maua.

Akizungumza wakati wa akifungua kongamano la kikanda la biashara la uwekezaji katika tasnia ya Mazao ya bustani lililoandaliwa na jumuiya ya wazalishaji wa mazao ya mbogamboga na matunda Tanzania (TAHA,) jijini Dar es Salaam. Majaliwa amesema kuwa TAHA na wadau wengine wa sekta hiyo waendelee kuishirikisha serikali katika kufungua fursa zote ndani ya nchi, katika Jumuiya za kikanda na kimataifa.

"Serikali imewekeza katika sekta ya kilimo kwa dhamira ya dhati na kila mtu akishikilie na hii ni kwa wakulima na wawekezaji....TAHA hamtabaki peke yenu." Amesema Majaliwa.

Amesema sekta hiyo ya kilimo cha mazao ya bustani ni muhimu sana na ilijidhihirisha wakati wa Covid-19 ambapo tiba mbadala ilikuwa ni kutumia mazao ya bustani ikiwemo viungo na mbogamboga jambo linalodhihirisha wazi umuhimu wa sekta hiyo.

Waziri Majaliwa amesema, serikali imefungua milango ya uwekezaji kwa wadau wa nje na ndani ya nchi na kuzitaka balozi kuingia makubaliano ya kibiashara katika nchi wanazowakilisha kwa kuangalia mahitaji ya bidhaa na masoko.

Pia ameiagiza Wizara ya kilimo kuunda Mamlaka maalumu itakayosimamia sekta hiyo ya mazao ya bustani pamoja na Wizara za fedha, Viwanda na biashara kutambua zao la Avocado kwa Kuhakikisha dunia inatambua Avocado inazalishwa Tanzania.

Vilevile ameipongeza taasisi ya TAHA kwa  uthububutu na kuwataka kuwafikia wananchi wengi zaidi katika maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA Dkt. Jacqueline Mkindi amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikitafuta fursa, masoko na kuhamasisha uwekezaji katika sekta hiyo ya mazao ya bustani.

Amesema, mazingira ya uwekezaji wa mazao hayo nchini ni rafiki na yenye sera imara na faafu yenye kuruhusu uwekezaji mkubwa katika mazao hayo na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo yenye soko kubwa ulimwenguni.

Dkt. Mkindi amesema, sekta hiyo inakuwa kwa kasi katika ukanda wa Afrika na ulimwengu mzima na kuiomba serikali kuendelea kushirikiana nao ili kuweza kufikia malengo ya kimaendeleo.

Aidha mwwnyekiti wa bodi ya jumuiya ya wazalishaji wa mbogamboga na matunda Tanzania (TAHA) Mhandisi. Zebadiya Moshi amesema serikali ya awamu ya tano inaonyesha jitihada katika kuboresha mazingira ya uwekezaji hasa katika kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na ameiomba serikali kuendelea kushirikiana na sekta hiyo yenye tija hasa kwa kutoa ajira kwa vijana.

Pia amesema kuwa, taasisi ya TAHA imekuwa ikitekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za kiufundi na kiutaalamu, utaalamu wa viwango lishe kwa wakulima pamoja na kutafuta masoko ndani ya nchi na katika kanda.

No comments:

Post a Comment