Nteghenjwa Hosseah - Singida


Mkurugenzi wa Huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr. Ntuli Kapologwe amepongeza Uongozi wa Kituo cha Afya Sokoine kilichopo Manispaa ya Singida Mkoani Singida kwa utoaji wa huduma bora za afya ya uzazi kwa akina mama na kuweza kuzalisha  akina mama 600 hadi 700 kwa mwezi. 


Dr. Ntuli ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya Timu ya Afya Mkoani Singida inayolenga kuhamasisha usimamizi shirikishi katika vituo vya kutolea huduma.


Amesema Idadi hii ya kinamama wanaojifungua hapa Sokoine ni kubwa na inatia moyo kuwa huduma mnayotoa ni nzuri na ndio maana wakinamama wanakimbilia kuja kujifungulia katika Kituo hiki cha Afya.


“Idadi hii ya akinamama wanaojifungua Sokoine inazidi baadhi ya Hospitali za Wilaya na  moja kwa moja inapelekea Kituo hiki cha Afya Sokoine kutoa huduma zinazolingana na za Hospitali ya Wilaya hongereni sana kwa kazi hii kubwa mnayoifanya” alisem Dr. Ntuli.


Akitoa Taarifa ya Kituo cha Sokoine kwa  Timu ya Usimamizi Shirikishi Mganga Mfawidhi wa Kituo Dr. Yuna Hamis  amesema tangu kuanzishwa kwa huduma ya upasuaji Mapema mwaka 2019 jumla ya akina mama 553 wamepatiwa huduma ya upasuaji. 


Katika kipindi chote hicho vifo vilivyotokea ni akinamama 3 na watoto wachanga 27, masirated 18 na FSB 9.


“Ongezeko la akinamama wanaojifungua limefanya mahitaji ya Kituo kuongezeka ikiwemo Idadi ya watoa huduma, majengo, dawa na vifaa tiba ambapo kwa sasa kuna jumla ya watoa huduma za afya wapatao 89” amesema Dr. Yuna.


Kituo cha Afya Sokoine ni miongoni mwa Vituo 44 vya awamu ya kwanza kupokea fedha za upanuzi wa Vituo vya afya nchini na kilipokea shilingi mil 500 kwa ajili ujenzi/ukarabati wa miundombinu ya kituo.


Sambamba na upanuzi wa miundombinu Kituo kimepokea vifaa- tiba vyenye thamani ya shilingi Mil 360 ambavyo kwa pamoja vimesaidiabkatika kuboresha Kituo na huduma za Kituo cha Afya Sokoine.


Kituo cha afya Sokoine kilianzishwa mwaka 1984, kikiwa na majengo matatu (Jengo la utawala, Jengo la wagonjwa wa nje na kliniki ya mama na mtoto, na hapo awali Huduma zilizokuwa zikitolewa ni huduma ya wagonjwa ya nje, afya ya uzazi na mtoto na kifua kikuu.


 Baada ya Serikali kufanya maboresho mbalimbali kwa sasa kituo kinatoa huduma Huduma ya tiba kwa wagonjwa wa nje, huduma ya kulaza wagonjwa, huduma ya afya ya kinywa na meno, huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya UKIMWI.


Pia Kituo cha Afya Sokoine kinatoa huduma ya kifua kikuu na ukoma, huduma ya afya ya uzazi na mtoto, huduma ya ustawi wa jamii, Huduma ya maabara, Huduma ya macho pamoja na Huduma za upasuaji na uongezaji wa damu kwa wagonjwa.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: