KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi) Dkt Rashid Tamatamah kulia akizungumza mara baada ya kukagua jengo la BMU Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yake ambapo aliridhishwa na kasi ya ujenzi wake  kushoto ni Mkandarasi wa Kampuni ya Stans Techinical Civili Engineer  Focus Ngowi 
Mkandarasi wa Kampuni ya Stans Techinical Civili Engineer  Focus Ngowi kushoto akimueleza jambo kuhusu hatua iliyofikia ujenzi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi) Dkt Rashid Tamatamah

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi) Dkt Rashid Tamatamah kulia akikagua ujenzi wa ofisi hiyo

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi) Dkt Rashid Tamatamah asema uvuvi harama kwa kutumia mabomu nchini umepungua kwa asilimia 100 huku kwa upande wa maziwa wakifanikiwa kudhibiti kwa asilimia 80.

Hatua hiyo imesaidia kuongeza uzalishaji wa samaki ambao wanazalishwa hapa nchini kutoka miaka ya nyuma mpaka sasa kutokana na udhibiti wa uvuvi haramu ambao umefanywa na serikali.

Dkt Rashid aliyasema hayo mjini Pangani wakati wa ziara yake ya siku moja ya kwenda kuangalia ujenzi wa ofisi za BMU Kata ya Kipumbwi huku akionyeshwa kuridhishwa na kazi ya ujenzi wake

Ujenzi unatekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya ufadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi unaoitwa Swiofish na unafanya mambo mengi huo lakini moja vitu ambavyo vimeazimiwa kutekelezwa vitu vya mwisho katika mradi huo wa miaka sita ambao utaisha mwakani.

Alisema katika vitu vya kutekelezwa ni kujenga majengo ya oifisi za BMU Tano kwenye ukanda wa Pwani walitaka kila mahali wajenge lakini fedha zilizopo zilikuwa hazitoshi hivyo wakachagua maeneo matano tu ambayo ni Lindi, Bagamoyo, Saadani, Kipumbwi na Zingibar

Alisema wakati serikali ya awamu wa tano katika kipindi chake ca kwanza ilipokuwa inanza kazi hali ya uvuvi nchini ilikuwa mbaya sana kutokana na kukithiri kwa uvuvi haramu.

Alielez baada ya serikali kuingia mwaka 2017 ikaamuliwa kwamba kama wataendelea hali hiyo ingeendelea rasilimali za uvuvi zingetoweka na kama unavyojua uvuvi ni moja ya sekta inayoajiri watu wengi wenye kipato cha chini kwa hiyo maisha ya watu yangebadilika.

 “Hivyo serikali ikamua kuchukua hatua za makusudia kuanzisha operesheni za uvuvi haramu kwenye maziwa waliita operesheni sangara na kwenye ukanda wa pwani kulikuwa na operesheni Jodari ambazo ziliwasaidia walikuwa wanawashirikisha BMU”Alisema Katibu Mkuu huyo.

 “Lakini pia na watu waliokuwa wanaitakia mema nchi yetu na taasisi za ulinzi na usalama hivyo baada ya mwaka mmoja matokeo yalikuwa mazuri sana kwenye ukanda wa pwani ikiwemo maeneo ya Kigombe na Tanga kwani uvuvi wa mabomu ulikuwa umekithiri kule Dar mabomu yalikuwa yakipigwa mpaka pale karibu na Ikulu”Alisema

Alisema operesheni hizo kwa upande wa pwani kuna meli za nje walikuwa wanapewa leseni za kuvua na ilikuwa ya mashati kwamba wavua samaki wa aina fulani lakini wakawa wanavua samaki ambao ni nje ya leseni.

“Kuna meli iliyokuwa inatoka Vetnam ilikamatwa ikiwa na mapenzi ya papa ilishikiliwa Serikali ikafungua kesi ikaendeshwa tukashinda ikapigwa faini ya Bilioni 1 au waende jela hiyo wameenda jela”Alisema

Akizungumzia upande wa Maziwa kwenye ziwa Victoria alisema wamefanikiwa kutokomeza uvuvi haramu kwa zadi ya asilimia 80 lakini bado hawajamaliza kabisa huko na kubwa zaidi ilikuwa ni matumizi ya nyavu haramu.

Alisema kutokana na kudhibiti uvuvi haramu mafanikio yake yamekuwa makubwa sana samaki wameongezeka kwa sababu mara ya kwanza wameweza kuvuka.

Alisema kwa sababu miaka ya nyumba kote Tanzania haijawahi kuwa na samaki ambao wanazalishwa Tani 400,000 ambazo zinazalishwa kwa mwaka ambazo zilikuwa zinazalishwa zilikuwa ni chini yake baada ya operesheni hizo kwa mwaka 2018/2019 kwa mara ya wamefika tano 448,000 huku mwaka uliopita walipata tani 497,000.

Katibu huyo alisema kwa upande wa ziwa Tanganyika samaki aina ya Sangara viwanda vingi vya minofu inayopelekwa nje ni vya Sangara hivyo kuna viwanda huko ambavyo vilifungwa kutokana na uwepo wa uvuvi haramu.

Alisema lakini pia zamani nchini walikuwa na viwanda vya Tanzania 12 hadi 13 lakini kutokana na uvuvi haramu nyingi vilikufa na kubaki 8 na vingi vilikufa kutokana na kukosa malighafi .

Aidha alisema kwani kulikuwa hakuna samaki na kupelekea viwanda ambavyo vilikuwa na uwezo wa kuchakata tani 40 kwa siku vilikuwa vinachangakata tani 3 mpaka 5 kwa siku kwa hiyo wafanyakazi ajira zilipotea.

“ Baada ya kufanikiwa kukomesha uvuvi harama samaki wanapatikana wameongezeka na sio tatizo viwanda vinazalisha muda wote na sasa kuna viwanda vinne ambavyo wanajengwa”Alisema

Hata hivyo alisema katika kipindi cha awamu ya tano wanaendelea kutoa elimu na wavuvi hawamu wengi wamebadilika na hiyo imewapa nguvu serikali ya awamu ya tano kipindi cha pili wajikite kwenye ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki na kiuchumi kuwawezesha watu wawezeke kwenye maeneo yote kuvua ambapo Rais Dkt John Magufuli amesema atanunua meli nane ambapo nne zitakuwa Zanzibar na nyengine zitakuwa huko Tanzania.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: