Tuesday, 10 November 2020

SURA HIZI ZINAWEZA CHOMOZA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI LA MAGUFULIWilliam Peter Ndilla.

Sumve, Mwanza,Tanzania.

November 10,2020.


Uteuzi wa kimkakati wa JPM kwenye Baraza lake la Mawaziri jipya unaweza kuendelea tena kama ambavyo ulivyoanzia ndani ya Chama Cha Mapinduzi wakati wa mchakato wa kutafuta Wabunge wa CCM mwaka 2020.


Kabla ya zoezi la utoaji fomu kwa Wagombea wa CCM,Rais John Magufuli aliwahi kunukuliwa akisema"....jipime na Uone unataka kuleta kitu gani kipya ambacho wengine hawana,....nahitaji watu Potential......".


Kauli hii ilikuwa sio kauli nyepesi na ilikuwa inaelezea jinsi gani uteuzi wa wagombea wa CCM katika majimbo ungekuwa wa kimkakati zaidi kuliko jinsi uteuzi ulivyokuwa huko nyuma.


Unapokuwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM  yenye kurasa mia tatu na tatu"303" hii ina maana kuwa Serikali ijayo itakuwa "imejicommit" pakubwa kwa hiyo unahitaji watu wenye maono makubwa,uzoefu mkubwa,elimu kubwa,na wenye ufanisi mkubwa kuweza kutekeleza Ilani hiyo.


Nilishawahi kusema kuwa Chama makini Cha siasa chenye malengo na maono ya mbali amacho kinataka kutengeneza Serikali inayo wajibika kwa watu wake lazima kiwe na sifa kuu tatu;


MOJA,Chama lazima kiwe na maono na malengo makubwa yanayobebwa na ideolojia ya Chama husika ambayo kwa neno rahisi tunaita Ilani"Party Manifesto".


Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020/2025 ya CCM ina jumla ya kurasa 303 na hii inawezekana ikawa Ilani ya kwanza kubwa kwa Chama Cha Siasa chochote barani Afrika kilichowahi kwenda kuomba kura kwa Wananchi kwa maana ya wingi wa kurasa.


PILI,Chama ambacho kinataka kuunda Serikali ya kutumikia watu lazima kiwe na uwezo wa kukusanya rasilimali fedha za kuwezesha kutekeleza maono na malengo ya Ilani husika.


Unapokuwa na Ilani yenye kurasa mia Tatu na tatu"303" lazima uwe ujipima msuli wako na uwezo wako wa kukusanya fedha kwa maana ya makusanyo.Hakuna Chama "Njaa" kingeweza kuwa na ubavu wa kuandika ahadi nyingi kiasi kile kama hauna uwezo wa kukusanya fedha.


TATU,hili la tatu ndio kubwa na Uti wa mgongo wa Chama na Serikali yenye maono ya kuwatumikia watu wake.Chama kinachotaka kuunda Serikali makini na wajibifu lazima kianze na usajili wa rasilimali watu wenye sifa za ziada za kutekeleza maono ya kiilani ya Chama."Party Internal recruitment and Selection of Candidates".


UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE NDANI YA CCM ULIKUWA WA KIMKAKATI.


Zoezi la kuteua wagombea Ubunge ndani ya CCM ulikuwa wa kimkakati sana japo Pamoja na kuangalia uwezo wa mtu pia uliangalia uwezo wa mtu huyo kukibeba Chama kwa maana ya ushindi.


Mimi ninaamini kwamba kama kusingekuwa na"Pressure" za Uchaguzi na ushindani, CCM ingeweza kuja na sura mpya nyingi na zenye uwezo zaidi kwa maana watu wenye kariba hiyo walikuwepo wengi.


Pamoja na hayo, mchakato wa Uteuzi ndani ya Chama kwa wagombea Ubunge na Udiwani ulizingatia sana mambo makubwa yafwatayo;


MOJA,rekodi za kipekee za mgombea katika eneo lake la Ubobezi na ndio maana hapa unamwona mtu kama Charles Kimei wa CRDB na Deo Mwanyika,Rais wa zamani wa Migodi ya Barrick Tanzania.


PILI,akili,maono na Uthubutu "aggressiveness" wa wagombea.Uteuzi ndani ya CCM safari hii uliangalia sana Vijana wenye akili kubwa,Maono makubwa na Vijana waliowahi kuthubutu kufanya mambo fulani walipopewa dhamana na Umma.


Kuna Kijana na Mteule wa Mufindi Kusini David Kihenzile,linaweza likawa jina jipya katika siasa za Tanzania lakini nilitegemea sana kumuona "akitoboa" na naona ana uwezo wa kutoboa ata katika teuzi zijazo.Tafuteni wasifu wa Kijana huyu ambaye kazaliwa Mwaka 1984 kwa hakika unavutia.


TATU,Utii na Uchapakazi wa wateule pia kilikuwa kigezo kimoja wapo cha Uteuzi ndani ya CCM mwaka huu.Hapa namwona Profesa Kitila Mkumbo ambaye rekodi zinaonyesha popote alipopita aliacha alama za wazi.


Nenda Wizara ya Maji na Uone mambo makubwa aliyofanya japo suala la Maji  linabaki kuwa changamoto lakini bado naona ndio mtu pekee wa kujibu hoja hii.Profesa anasifika tangu akiwa Chuo Kikuu kwa Uchapakazi na Utii.


NNE,Uwezo wa kukipa Chama ushindi pia ilikuwa miongoni mwa sifa kuu ya wateule wa awamu hii.Mfano mzuri ni katika Jimbo langu la Kyela ambapo na Mimi nilikuwa Mgombea.


Kwa Siasa za kyela zilivyokuwa mtu pekee ambaye angekivusha Chama alikuwa ni Jumbe Ally Mlaghila"Kinanasi" vinginevyo CCM ingepata wakati mgumu sana!


UTEUZI ULE WA KIMKAKATI NDANI YA CHAMA ULILENGA KUUNDA BARAZA LA MAWAZIRI LA KIMKAKATI.


Uteuzi wa Wabunge ndani ya CCM ulikuwa na malengo makubwa mawili,kwanza ilikuwa kuja kuunda Serikali makini na pili kuunda Bunge makini ili kuwepo na dhana nzima ya "Compactness".


"....nileteeni Gwajima,nileteeni Gwajima,..nileteeni Gwajimaaaaa....".Rais Magufuli alisikika akisema katika moja ya mikutano yake ya Kampeni Jijini Dar es salaam.


Kauli hii ya Mh.Rais haikuwa ya Kawaida ata kidogo bali ilikuwa ya Kimkakati kuelekea Uundwaji wa Baraza la Mawaziri na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kuonyesha kuwa Mh.Rais kuna aina ya watu ambao aliona watamfaa "mbeleni",kwenye baadhi ya Maeneo ilibidi apige mkwara kidogo,mfano Mkoani Songwe,Wilayani Momba,Jimbo la Tunduma.


"...Kama Mnataka Maji nileteeni Silinde,...siwezi nikapeleka Maji kwa mtoto wa Jirani....."


JE,KWANINI MH.RAIS ALIONEKANA KUWAPIGANIA WAZIWAZI WAGOMBEA FULANI FULANI?


Jibu ni rahisi sana,Rais  Magufuli na wagombea hao "wana Jambo lao wiki hii".Nadhani ninaeleweka.


Sitaki kutaja majina ya nani atakuwa nani kwani huko kutakuwa kuingia kwenye kichwa Cha Mh.Rais na Mamlaka ya Uteuzi ambavyo kwa mujibu wa Chama Chetu ni Mwiko.


Nimtakie Mh.Rais afya njeema na akili na ufahamu kutoka kwa Mungu ili afanye Uteuzi kwa kuongozwa na Mungu kama ambavyo amekuwa akifanya teuzi zake kwa kuongozwa na Mungu wakati wote.


+255759929244

Willum Peter Ndilla 

Aliyekuwa mgombea Sumve na mpenda maendeleo wa Nchi yangu Tanzania 🇹🇿

No comments:

Post a Comment