MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akila kiapo cha kuwa mbunge Bungeni
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kushoto  akila kiapo cha kuwa mbunge Bungeni
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira waliosimama nyuma wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya Pamoja na Rais Dkt John Magufuli aliyekaa katikati kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu na kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira waliosimama nyuma wa nne kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya Pamoja na Rais Dkt John Magufuli aliyekaa katikati kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu na kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai ,Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na kwanza kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Haasan Mwinyi
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akimpongeza Waziri Mkuu Kasim Majaliwa bungeni Jijini Dodoma kwa kupata kura za kishindo asilimia 100 kuthibitishwa na bunge kuwa Waziri Mkuu




NA MWANDISHI WETU, DODOMA.

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira amesema hotuba ya Mhe Rais Dkt John Magufuli imemgusa baada ya kuona namna alivyogusia makundi yake ya kipaumbele cha kwanza uwezeshwaji kiuchumi wanawake na mikopo isiyokuwa na riba na yenye riba unafuu.

Neema aliyasema hayo ikiwa ni muda mchache mara baada ya Hotuba hiyo ya Mhe Rais Dkt John Magufuli wakati akilifungua Bunge la 12 jijini Dodoma ambapo alisema pia imewagusa wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wazee.

Alisema pia aligusia kwa mapana mambo ambayo serikali yake kwa kipindi cha muhula wake wa pili itakayokwenda kuifanya kwa ajili ya wazee hali iliyompa faraja kuona nafasi yake binafasi tayari kwa kuchangia kikamilifu kwenye utekelezaji wa Ilani ya CCM na dira ambayo Rais amewapatia.

“Lakini pia nimeguswa na mpango mkakati wa serikali kwenda kuboresha mazingira wezeshi ya biashara kwa nia ya kuongeza uwekezaji ambao utapelekea kuongeza ajira na kuinua uchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”Alisema

Aidha alisema kwamba hotuba hiyo imemfariji maana amegusa kwa ukamilifu sekta ya kilimo na umuhimu wa kuunganisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na sekta binafsi.

“Kama unavyofahama masuala mengi yanayofanywa ngazi ya jamii yanafanywa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na asasi za kiraia hivyo mimi kama mwakilishi wa NGOs Bungeni kitu cha kwanza ni kuanza kuzitambua NGOs kwenye maeneo hayo ya kipaumbele ambayo Mhe Rais amewaambia leo yanafanya nini” Alisema

Mbunge huyo alisema pia ataweka kipaumbele kikubwa kuelewa wafadhili wa NGOs hapa Tanzania na wadau wa maendeleo wanafadhili kwenye maeneo gani kisha waone hayo maeneo wanayofadhili kama yanaenda sambamba na dira ya serikali na dira ya Mhe Rais.

“Lakini kama hayaendani sambamba nini kifanyike kwahiyo mimi nitakuwa kiungo kati ya mashirika yasikuwa ya kiserikali, bunge na serikali pamoja na wafadhili” Alisema

Mwisho.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: