Wednesday, 21 October 2020

WILAYA ZA WAFUGAJI HATARINI KUKOSA MALISHO YA MIFUGO.

 


NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA 


Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanta amesema wilaya za Longido, Monduli na Ngorongiro zipo hatarini kukosa malisho ya nifugu kutokana na athari za gugu vamizi la gugu karoti linaloua malisho na kuharibu ardhi.


Kimanta aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya kutokomeza gugu karoti mkoa wa Arusha  ambapoa alisema kuwa gugu hilo ambalo mche mmoja una mbegu elfu 30 linaendelea kuenea kwa kasi na kuleta madhara kwa malisho hali itayopelekea mifugo kufa.


"Kama mifugo itakufa kipato cha wananchi kitapungua na hii itapelekea pia kodi za serikali kupungua kwahiyo kama serikali ya mkoa nitatafuta njia nzuri ya kupambana na gugu hili" Alisema Kimanta.


Alifafanua kuwa serikali ni lazima iunge mkono jitihada zinazofanywa za kutokomeza gugu karoti ambapo atatengeneza mnyororo wa kutokomeza kwanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa.


Aliendelea kusema kuwa katika kila kikao atahakikisha wanazungumzia gugu hilo ili kusaidia  jamii kupata uelewa na kuanza kupambana nalo kwani bila kuwashirikisha hawataweza.


Aidha alizitaka taasisi za kitaalamu kushirikiana kuona ni namna gani wataweza kuliondoa gugu hilo ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi kwani ushindi wa vita dhidi ya gugu hilo ni wananchi wenyewe.


Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti gugu karoti mkoa wa Arusha Ndeelekwa Kaaya alieleza kuwa gugu hilo liliingia hapa nchini mwaka 2010 ambapo madhara yake ni makubwa kwa afya za watu, mifugo, mimea pamoja na ardhi.


Kaaya alifafanua kuwa kwa binadamu endapo atagusa gugu hilo ataharibika ngozi, na kupata aleji itayopelekea kupata kikohozi kikavu kutokana na hewa itayotoka katika kuku hilo na kuingia kwake.


Alifafanua kuwa kwa upande ng'ombe asilimia zaidi ya hamsini anaathirika kwanzia mdomoni kwa kupata vipele na  kung'ooka meno, maziwa kupoteza rangi na ladha.


Pia alieleza kwa upande wa kilimo na malisho gugu hilo linaua miea iliyopo karibu pamoja na kuharibu udongo kutokana na kuwa na sumu inayoua virutubisho vilivyopo katika udongo.


Mmoja wa waathirika wa gugu hilo  Elinuru Moses Pallangyo alisema kuwa alitumia gugu hilo bila kujua kuwa ni hatari ambapo aliyakuta katika shamba lake la karoti ambapo aliyachukua na kuwapa ng'ombe na baadae akakuta ng'ombe wake wamekufa 


"Baada ya ng'ombe kufa sikujua nini chanzo lakini baadae pia na mimi nilianza kuvimba mikono na uso, kubanwa kifua pamoja na mwili kukosa nguvu"Alisema Elinuru.

No comments:

Post a Comment